Mwanabongofleva aliyewahi kutamba kitambo kwa albamu yake kali ya Starehe iliyobebwa na nyimbo kibao kabla ya kupotea na kurudi ameachia wimbo mpya unaoitwa Nimejifunza.Wimbo huu umebeba mambo mengi aliyopitia na alivyojifunza juu ya marafiki wa kweli na wasio wa kweli.
Wimbo umetayarishwa kwenye studio za Mkubwa na Wanawe na Shirko. Kwa
sasa muimbaji huyo yupo chini ya Said Fella aliyeshiriki kuuandika.
Usikilize hapo chini na kuudownload.