Baada kufungiwa kujishughulisha na shughuli za sanaa kwa kipindi cha
mwaka mmoja, mwanadada Shilole ameibuka na kuongea haya; “Mnataka
nikaishi wapi nina familia ya watu 10 ndani, nina watoto 2 wanaosoma
boarding kila mwaka ninatakiwa nilipe mil 5 kila mmoja, nina watoto 3
yatima ninaowalea wanasoma vilevile, kupitia muziki huu huu ninaofanya
ambao watu wengine mnaudharau lakini ndio unaonifanya nifike hapa,
ninalipa kodi ya nyumba Mil 7 kwa mwaka, ninalipa kodi ya maendeleo ya
nchi yangu na bado nina watu ninaowasaidia”