Msanii wa Bongo Movies, Adam Haji ‘Baba Haji’ aliangusha sebene la
nguvu kwenye Viwanja vya Ngome Kongwe, Zanzibar baada ya kupata taarifa
kuwa Wema Sepetu aliyekuwa akiwania nafasi ya ubunge wa viti maalum
mkoani Singida kwa ‘leseni’ ya CCM, ameangushwa.
“Jamani mmesikia
majibu? Mbunge wenu kashika nafasi ya mwisho, ngoja mimi niendelee
kucheza sebene langu,” alisikika Baba Haji huku akiangua kicheko.
Source: GPL