Akiwa
nchini Afrika kusini msanii machachari sukari ya warembo, raisi wa
WASAFI amepata nafasi ya kukutana na wasanii wengine wa hapa Afrika na
kutoka mabara mengine ambao wako nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya
kushuhudia na kutumbuiza katika tuzo za muziki za MTV ambazo Diamond pia
ni mmoja ya washiriki. Baada ya kupiga stori na D Banj ndipo Diamond
alipopewa taarifa ya kuwa anatafutwa na msanii NE-YO kutoka nchini
marekani na kufanikisha kuonana nae na kupiga stori kadhaa ambazo bado
hajaziweka wazi kuwa ni kipi hasa ambacho wakali hao wawili walikuwa
wakiteta.