Siku zote wanasema kizuri kinajiuza chenyewe, ni katika harakati za kusaka mziki mzuri masikioni mwangu nikakutana na huu wimbo kutoka kwa Buoywonda maskani yake Kenya, kwa kweli sikukiamini ila ladha niliyoipata masikioni mwangu, melodi tamu, mashairi yamepangika na kila kitu kizuri kiko humu. Nikaamini ule usemi usemao avumaye ni papa kumbe na wengine wamo.
Hebu nawe sikiliza wimbo huu mtumie na rafiki yako ili tuweze kukuza vipaji hivi ambavyo ni tunu kubwa sana Afrika mashariki na dunia kwa ujumla, tumpe sapoti kijana ili aweze fika mbali.