Wasafi Records ambayo wao hupaita House Of Hits (H.O.H) ndipo zilipotoka nyimbo kali zaidi katika chati za bongo. Ukizungumzia mziki wa Tanzania kwa sasa mtu wa kwanza kumtaja nadhani atakuwa ni kijana mwenye juhudi na maarifa makubwa katika mziki aliyeitangaza Tanzania duniani kote kupitia mziki wake, Naseeb Abdul ama kama wengi tulivozoea kumuita Diamond Platnumz likiwa ndio jina lake katika sanaa ya bongo. Wasafi records ni studio inayomilikiwa na Diamond platnumz akiwaongoza wasanii kadhaa ambao wamesaini chini ya label yake ya WCB akiwemo Harmonizer, Raymond, na wengine ambao bado haijawekwa wazi ila kunatetesi pia wameingia mkataba na lebo hiyo ya wasafi akiwemo mkali wa kurap Young Killer Msodoki handsome boy asiye na matunzo pamoja na Rich Mavoko ambaye hivi karibuni inasemekana alikuwa na Chibu huko kwa madiba kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake mpya.
Hadi sasa Wasafi records imeshafanya nyimbo na wasanii wengi sana wa Bongo na nje ya Tz ambazo zote zimeonekana kukukimbiza katika chati mbalimbali za mziki wa bongo kwenye TVs na redio, vyombo vya habari vya nje ya Tz kama MTV na Trace.
Baadhi ya matangazo na nyimbo zilizofanyika katika studio hiyo ni:
- NATAFUTAKIKI
- BADO
- KWETU
- SWEETLOVE
- VODACOM ONGEA DEILEE
- COCACOLAOnjaMsisimko
- REDGOLDLadhaNaMtonyo
- NAMJUA
- Colors Of Africa
- UTANIPENDA
- ZIGORemix
- AIYOLA
Pia kama unakumbukumbu nzuri mwaka jana ulikuwa ni mwaka uchaguzi hapa Tanzania, ambapo kampeni zake zilikuwa ni za aina yake kwani zilitawaliwa na michuano mikali ya wanasiasa. Wanasiasa waliwatumia wasanii kwa kiasi kikubwa kupata mafuasi wengi zaidi ikiambatana na burudani zilizokuwa zikitolewa katika majukwaa ya siasa. Wasafi records hawakuwa nyuma wakiongozwa na Chibu mwenyewe waliandaa nyimbo tofautitofauti zilizotumika katika kampeni hizo ikiwemo
