Mabaga Fresh Vs Gangwe Mob, Tanzania Hip Hop Dis

Chanzo cha beef kati ya Mabaga Fresh na Inspector Haroun
Kwenye miaka ya 99 Mabaga Fresh waliandaa show katika ukumbi mmoja wa burudani uliopo Temeke na waliwaalika wasanii wengine wengi wakiongozwa na Gangwe Mobb, ambao enzi hizo walikuwa wanawika na ngoma kadhaa kama Ngangari, Mauzauza na MtuBee. Makubaliano yalikuwa malipo yatategemea na idadi ya watu watakao ingia kwenye show.


Basi bwana, Kama zali vile Show ilitema mbaya, mtu shazi zilihudhuria show, ila sasa kwenye malipo bwana daaah!
Mabaga Fresh wakawaambia Gangwe Mobb kuwa wao wamepata hasara, Show imekula kwao kwan mapato yote wamelipia ukumbi na mambo mengine, lakini hawakuwaacha mkono mtupu,wakawalipa Shilingi Mia Tano ( Jero).

Gangwe walimind sana lakini Inspekta alimaind zaidi na Cha zaidi hapo ni kwamba Kuanzia siku hiyo Mabaga Fresh wakawa Paka na Chui na Gangwe Mobb ingawa wote walikuwa kwenye koo la WALUMENDAGO iliyokuwa na makundi mengine mengi Kama FSG(Nature + Dollo), Kamili Gado Crew,Joint Mob, Boyz from ze Army nk

Haikuwa rahisi kwa Gangwe kuwachenjia Mabaga 1kwa1 hasa wakihofia jamii vile ingewachukuliaje kwani Mabaga walikuwa ni walemavu walioamua kufight kupitia muziki na jamii iliwatazama kama mfano, pamoja na hayo Inspector tofauti na wenzake  yeye aliumia saana na akawa analalamika sana kwa masela kwamba jamaa wamepiga mkwanja af ndio vile tena juu kwa juu.

Habari za lawama zikawafikia Mabaga, wakajiuliza mbona Dogo anachonga pembeni badala ya kuwafata direct na kusema nao, kuona hivyo ndio sasa wakaamua sasa "KUMTULIZA" Inspector na ndio wakaja na "MTULIZE" na tena wakamshirikisha JumaNature ambaye kwa kipindi hicho nae alikuwa anabeef na Inspector

Katika wimbo Mtulize ambao Mabaga Fresh waliurekodi kwa mara ya mwisho (Walishaurekodi zaidi ya mara mbili ) mwaka 2000 kuna mistari inasema..

 Twenzetu
J.B (Yule mwenye sauti nyembamba ) anasema " MBELE YA CHOMBO CHA DOLA HAKUNA CHA NGANGARI"(Hapa ana diss wimbo Ngangari wa Gangwe Mobb)

Mstari mwingine, DJ SNOXX ( Yule mwenye sauti nene ), anasema; "NGEDERE NIAZIME SURA YAKO NIMTISHIE MWANANGU".
Hapa DJ SNOXX ana mock muonekano wa sura ya Inspector Haroun kwa kumfananisha na ngedere na mistari mingine kibao ambayo inspector nae akaja kuijbu katika Wimbo wa Zay B NIPO GADO(Original.)

Source: WhatsApp