Diamond Platnumz kama Husein Bolt, aivunja rekodi aliyoiweka mwenyewe

By    
 
Kama unakumbukumbu nzuri basi utakuwa hukupitwa na ile stori iliyopamba vichwa vya habari kila kona ya video ya msanii Diamond Platnumz aliyowashirikisha wasanii Peter and Paul maarufu kama P Square na wimbo wa KIDOGO ambayo ndani ya siku nne tu iliweza kupata watembeleaji zaidi ya milioni moja. Sasa video yake mpya ya Salome aliyoianya na Rayvany kutoka lebo yake wa WCB imeweza kuvunja rekodi ile aliyoiweka mwanzo katika mtandao wa YOUTUBE na kujipatia waonaji zaidi ya milioni moja kabla hata ya siku nne.