Star wa muziki Barnaba, amejinadi kuwa albamu yake mpya itaingia sokoni
kwa bei ya dola 100 ama zaidi, pesa ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi
laki 2 za Tanzania kwa nakala 1.Mkali huyo amekuwa akijiamini kutokana
na ubora wa nyimbo, utofauti na uwekezaji mkubwa anaoendelea kuufanya
kukamilisha kazi hiyo.Barnaba ameeleza kuwa, baadhi ya rekodi kutoka
albam hizo zimekwishapelekwa nchi mbalimbali ikiwepo Afrika Kusini na
Ujerumani kwaajili ya 'Mastering', zikitarajiwa kutoka kwa mfumo wa DVD,
na vile vile CD za kawaida, kwa bei hiyo ambayo hata hivyo amesisitiza
kuwa inaweza kuongezeka zaidi.
Source: EATV