July 5, 1982 Ambwene Yessayah alizaliwa. Namshukuru Mungu kwa kuiona
siku hii ya leo. Nawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani. Mungu
awalaze mahali pema peponi. Natamani
mama yangu angekuwa hai aone jinsi kijana wake alivyokuwa mkubwa na
pengine afurahie jasho lake la kunizaa, kunilea na kunitunza.
Nawashukuru wote walio na mchango mkubwa kwenye maisha yangu, ni wengi
siwezi kuwamaliza kuwataja. Navikushukuru vyombo vya habari vyote kwa
support kubwa inayoendelea kunipa. Nakushukuru pia wewe shabiki yangu
kwa kuendelea kuniunga mkono. Thank You!!