Baada mwanamitindo na msanii Jokate kuandika ujumbe mzito kwa Diamond
Platnumz na kumshutumu kwa kuweka video inayomuonyesha akicheza wimbo wa
“Mdogomdogo” Diamond alipoongea na 255 ya Clouds Fm alimjibu kwa kusema
haya.
Diamond amesema “Mimi nimempost kama fan wangu, ile caption yangu
sijamuandika jina kwanini achukulie vibaya, ukiona mtu anajishuku ujue
kuna namna nyuma, mbona mimi napost watu wengi na caption zangu za
vituko vituko manaake mimi nina caption za vituko mi ni mswahili
nimezaliwa tandale nimekulia tandale na tandale ndo imenifanya niwe hapa
nilipo, kuna caption zangu za uswahili coz uswahili ndio umenikuza
mpaka kuwa fame, mbona naandikaga kwenye caption kwann kwake yeye ndo
tatizo kwani kuna ubaya gani kuandika mtanyooka tu kama haimuusu,maana
ukiona hivyo ujue kuna kitu kinamuhusu, yeye mpaka nimeenda kuchukua
tuzo amesapoti nini, alipost hata post moja ya kusema mpigie kura
Diamond, anajishaua eti nimesapoti kasapoti nini.”