Video hii mpya inayongojwa kwa hamu sana na mashabiki na maadui wa msanii Ali Kiba imepikwa na Meji, muongozaji wa video za muziki wa Nigeria aliyoongoza video za wasanii wakubwa wakiwemo Asa – Eyo, Seyi Shay – Crazy (ft Wizkid), Asa – Satan Be Gone, Who Is Ugo Mozie, The Thirst – Today, Seyi Shay – Murda (ft. Patoranking & Shaydee) na wengine wengi.
Imekuwa ni mtihani mkubwa sana kwa Kiba kutokana na ushindani uliotengenezwa na Team mbili kubwa hapa Bongo ni ile ya Kiba na ya Diamond ambazo kila moja iko macho usiku na mchana kuangalia mwenzake anafanya nini na anakosea wapi ili kutengeneza stori za mtaani.
Nadhani Kiba ashaweka mambo sawa kama unavyoona hapo chini katika picha.
Alikiba akiwa location wakati wa kushoot video ya Chekecha
Msafara mzito
via