Kama
unavyoiona hapo juu hiyo ilikuwa ni siku za nyuma zaidi ya miaka miwili
iliyopita, hakukuwa na tofauti kati ya wasanii hawa waili Diamond na
Ali Kiba na kama zilikuwepo basi zilikuwa ni za chinichini kiasi hata
mashabiki hawakuweza kuzijua na isitoshe kwa wakati huo hakukuwa na
ushindani mkubwa kati yao kitu amacho ni tofauti na sasa kila mmoja
anataka kuwa juu ya mwenzake na kuonekana yeye ni bora zaidi kuliko
mwenzake.
Hadi
sasa bado imekuwa ni utata mkubwa juu ya wasanii hawa vinara kabisa
hapa nchini na kusababisha mgawanyiko mkubwa sana wa mashabiki kitu
kilichopelekea kuzaliwa kwa timu mbalimbali za ushabiki wa mziki wa
Bongofleva ambazo zimekuwa zikizidi kushika kasi huku kila timu
ikijitahidi kuuandika vibaya upande mwingine ilimradi tu kufanya timu
yake na mtu wake aonekane yuko juu zaidi ya mwenzake.
Wadau
na wasanii mbalimbali wameonekana kukerwa sana na timu hizo kwani
zinapelekea kuwaingiza na wasanii na wadau wengine katika ugomvi huo,
mfano Davido kutoka Nigeria alikereka na Timu Kiba ilipoonekana kujaza
maneno ya kumdhihaki msanii Diamond katika ukurasa wake katika
kinyang'anyiro cha tuzo za MTVMAMA 2015. Pia wasanii Aika na Nahreal
Mkono kutoka kundi la Navy Kenzo wameliongelea suala hilo katika upande
hasi masaa machache yaliyopita katika kituo cha luninga cha EATV.
MUNGU
AWAJAALIE WASANII HAWA WAWILI WAWEZE KUKETI CHINI NA KUZIMALIZA TOFAUTI
ZAO KWANI NAAMINI NI WAAMINI SAFI WA DINI NA DINI SIKU ZOTE HUIMIZA
UPENDO.