Kama ni mfuatiliaji mzuri wa mziki habari za town basi utakumbuka kuwa wikendi hii msanii Mabeste alifanya tukio maalumu pale MAISHA CLUB ambapo pesa iliyopatikana katika show ile ni kwa ajili ya matibabu ya mke wake LISSA ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi kwa muda sasa.
Kuambatana na tukio hilo Msanii Mabeste kaamua kuachia wimbo maalumu kwa ajili ya Mke wake ambao rasmi utatambulishwa katika kituo cha Redio cha Clouds FM leo kutokana na taarifa tuliyoipata kutoka kwa Adam Mchomvu moja ya watu wa karibu wa msanii huyo.
"#Tune #XXL Mabeste leo ataachia New Single maalum aliyomwimbia mkewe LISA utaiskiliza #Exclusive hapa!!" - XXL Clouds Fm Radio
STAY TUNED SIKILIZA MDUNDO ITAKULETEA WIMBO HUO SOON UKIWA RELEASED