Nyimbo hizi Diamond hawezi zisahau kamwe

By    
endofvid [starttext]
Na.Mwanakalamu
Diamond ni habari ya Afrika, ametoka kufanya matamasha ya muziki makubwa barani Ulaya na Marekani na kuteka hisia za wapenzi w muziki wake kila anapotumbuiza.
Ametoka wapi huyu Milionea ambaye kila akanyagapo panageuka dhahabu?
Mwenyewe anasema ''From Tandale to the World''.
Naam katoka Tandale ambako ''alihaso' sana kabla ya kutoboa , alianza kwenye sifuri hadi kwenye tunayoiona mia ila kwake anaweza akasema ndo kwanza yupo arobaini, nani alikuwa anajua kuwa angefika alipofika?
Naamini hayupo na kama wapo basi ni wachache sana na huenda hao wachache walikuwa wakimwombea tuu hayo ama wakiota, lakini ni kweli amefika ambapo kwa jicho na akili ya kawaida hakuna ambaye angewaza.
Alipochukua tunzo nyingi Bongo angebweteka lakini hakufanya hivyo akapiga hatua, alipotajwa kuwania tuzo za BET angejisahau lakini alikaza mwendo na hata alipochukua AFRIMA ahakusimama na hatimanye tunzo hizo zikamzoea akazibeba za kutosha na Mtv nazo zikaweka kambi kwake, lakini hajasiama leo hii kavuka mabara , anafahamika kwote huko na bado anapiga hatua.
Najua ni funzo kwako kijana na hata mzee unayeridhika , kwa kidogo tuu ukipatacho.
Kama nilivyosema awali , kijana huyu alianzia sifuri ambako ni watu wa mtaani kwake na mitaa ya jirani pekee ndip waliojua kipaji chake hadi alipofika leo , leo tutaangalia nyimbo kumi ambazo daima atakuwa akizikumbuka na kuziwekea uzito kila akizisikia.

1.KAMWAMBIE
Huu ni wimbo ambao ulitufanya wapenzi wengi wa muziki tumtazame kijana huyu kwa jicho la ziada.Ulikuwa ni wimbo wa nguvu ambao bila shaka hautosahaulika kichwani mwake kwani ndio ulimtengenezea njia nchini na hata nchi za jirani zinazotumia kiswahili.

2.MBAGALA
Kikawaida mwanamuziki hupimwa na wimbo wa pili kama kweli anakipaji ama alibahatisha wimbo wake wa kwanza.Lakini Diamond alithitisha kipaji chake kwa wapenzi wa muziki kwa kutoa wimbo huu ambao uliikamata Afrika mashariki na kumfanya atazamwe kama moja ya wasanii wakali ambao walikuwa wanakuja kuikamata Tanzania.
Wimbo huu pia ulimfungulia njia ya kimataifa kwani ulifanikiwa kuingia kwenye kuwania tunzo za muziki za Mtv licha ya kutoshinda.
Bila shaka yoyote utakuwa umebaki kwenye kumbukumbu zake daima.

3.NALIA NA MENGI 
Wimbo huu ambao aliuimba na Rapa Chid Benz ulionekana kubeba hisia nyingi za maisha yake na ujumbe mzito.Nadhani historia ya maisha yake ilimsukuma kuandika wimbo huu ambao licha ya kutotamba sana redioni ulibaki kwenye 'playlist' za watu wengi wakiusikiliza ujumbe huo.
Kwa kubeba historia yake ya maisha daima wimbo huu hautosahaulika kwake.

4.MOYO WANGU
Yaap! hapa ndipo patamu, ilikuwa ni baada ya kutoka kwa Bob Junior ambako alikuwa ameshatengeneza albam nzima , lakini matatizo katika kutengeneza wimbo wa gongo la mboto yakamfanya kijana huyu kutoka Mbagala ajiongeze na kuanza kurekodi kwingine na akaanza Fishclub kwa Lamar ambaye kwa kipindi hicho alikuwa moto wa kuotea mbali.
Moyo wangu licha ya kuonekana ni wa kawaida mwanzoni ulikuja kuikamata Afrika mashariki na kuwa moja ya nyimbo bora kuwahi kutokea kutokana pia na ubunifu wake kwenye video.
Bila shaka wimbo huu ulikuwa ni mwanzo wa mabadiliko ya kimtazamo wake katika muziki na kuwa moto wa kuotea mbali.

5.NUMBER ONE 
Wimbo huu unaweza ukawa ulimlipa na kumpooza mateso aliyokuwa amepitia kwani ulimpa nguvu ya kuvunja rekodi katika tunzo za muziki za Kili na kumfungulia vizuizi vingi vya kimataifa nakisha kumuweka juu.
Number one wimbo ambao huenda kila akiusikia anajikuta akicheka sana kwani ulipelekea kufanyika kitu ambacho nacho huenda hakukifikiria awali.

6.NUMBER ONE REMIX
Huu ni zao la number one ambao aliamua kufanya na Davido ambaye ni kama walicheza bonge la kete kwani Davido akajenga ngome Bongo na Diamond akatoboa.
Wimbo huu ukampa tunzo na njia zaidi za kwenda mbele kimataifa na 'koneksheni' nyingi zilianzia hapa.
Diamond Plutnumz akiusikia huu wimbo huenda akafungua jokofu na kuchukua maji ya baridi na kuyanywa maana anaweza furahi hadi akazidiwa.

7.MDOGO MDOGO
Nilipofanikiwa kuiona 'Behind scene' ya video ya wimbo huu, ilikuwa ni zaidi ya kutafuta, hapo nilimwona Diamond ni mtu wa tofauti na wa ajabu sana , licha ya jina lake na mapesa aliyokuwa nayo alikubali kupigwa na baridi kali la mji mmoja aliopo Afrika kusini ili tuu atengeneze video ya wimbo huu.Hakika yalikuwa mateso angeweza kumfanya mtu mwingine achukue uhusika wa mahali pale ambapo ilimpasa kuteseka ,lakini aliamua kuifanya kazi kwa ukomavu wa hali ya juu na hatimaye wimbo huu uliweza kumuweka kwenye 'levo' za juu barani Afrika.
Akikumbuka lile baridi lazima anyooshe miguu na kucheka kwa furaha.

8.NITAMPATA WAPI
Ni kati ya nyimbo kubwa zilizoweza kumpatia tunzo nyingi za muziki ndani na nje ya Tanzania.Mashairi yake mazuri ,melody kali na video ya kuvutia viliufanya wimbo huu kuwa moja ya nyimbo nzuri barani Afrika ambapo licha ya tunzo ulikuwa ukimpa michongo mingi ya matamasha.
Kweli kwake tatizo halikuwa nyota.

9.NANA 
Nana ni wimbo ambao kikawaida tulitegemea ungekuwa ukishindania tunzo mwaka huu lakini mara tuu ulipotoka ulianza kuzoa tunzo nyingi za nje ya nchi.Nana ni moja kati ya nyimbo ambazo huenda alipozitoa hakutegemea makubwa sana lakini wimbo huu umevunja rekodi nyingi ambazo zitamfanya asiusahau.

10.MAKE ME SING 
Ulikuwa kama wa kawaida alipoutoa lakini ghafla ukaeleweka na sasa ni moto wa kuotea mbali.Ni wimbo mkubwa si Afrika tuu bali hata alipofanya matamasha nje ya Afrika wimbo huu ulioneke]ana kuwavutia wengi, naamini utakuja kushinda tunzo nyingi za muziki ndani na nje ya Afrika.
Hawezi kuusahau kwani ni motoooo.

Kuna nyimbo nyingi ambazo Diamond Plutnumz hatozisahau lakini hizi ni baadhi ya nyimbo ninazoaminin kutokana na kuwa na historia na mafanikio mbalimbali zitabaki kichwani mwa mtunzi daima.Kumbuka haya ni maoni na mtazamo wangu na si maoni yake na huenda tukatofautiana kabisa nimejaribu tuu kubashiri kwa kusoma matukio na nyakati.
[endtext]