SUALA LA MSANII WA KIZAZI KIPYA DIAMOND PLATINUMZ KUONYESHA NGUO ZA NDANI LINAMAANA GANI KWA MASHABIKI WAKE

By    

Mimi ni mmoja kati ya wadau ambao husifia sana kazi za Diamond. Ni kweli amekua akifanya vizuri kwenye Audios, Videos, hata live performance. Ila kwa hili tukio alilolifanya kwenye Fiesta 2012 ndani ya Leaders Club nimeshindwa kuelewa alikua na nia gani. Huwa sipendi kumlaumu mtu moja kwa moja sababu huwezi fahamu nini hasa kilimpelekea kufanya hiviyo. Ila kwa haraka  haraka naweza sema hakutumia busara kufanya hivyo jukwaani.

Maswali nijiulizayo:-
  1. Alikua anatangaza biashara ya mavazi hayo baada ya kuahidiwa pesa nyingi?
  2. Aliamua kufanya hivyo kupagawisha mashabiki?
  3. Pombe au kilevi chochote kingine ndicho kilimpelekea kufanya hivyo?
NB:Kwa nchi za ulaya suala kama hili si la ajabu kwani wasanii kibao wamekua wakifanya hivyo, lakini kwa suala la kitanzania bado haijazoeleka kitu kinachoweza kufanya msanii huyu ambaye kwa sasa ndiye anae make headlines kwenye magazeti mbalimbali kupoteza idadi kubwa ya mashabiki wake.