KITELEPHONE ASHA NGEDELE

By    
Mimi kama MOBILE PHONES REPRESENTATIVE nimepokea malalamishi yafuatayo kutoka kwa simu yako.... Nitaipresent kama nlivyoipokea....
MIMI KAMA SIMU YAKO:

1. Nataka uniheshimu nikuheshimu, yaani tuheshimiane. Sipendi kila saa ukiniweka katika vibration mode, utaki mie niimbe mbona, tena hasa ukiwa na huyo kibaby chako, kama unajiamini VIBRATION ya nini?!?
2. Usiweke kwa mfuko ya nyuma, kwani ukiachia KIBOMU (ukichafua hali ya hewa) wataka mi ndo nivute HARUFU yako?!? Na mambo ya kunichanganya kwenye wallet yako au mfuko na LESSO yako hiyo usiyowahi ifua toka ununue acha!!! Utaniambukiza MAFUA BUREEEE...
3. Ukiamumka asubuhi please brush mdomo ndio uanze kunitumia... Kwa taarifa yako mdomo unanuka! Huwa sitaki 2 kukuambia!!!
4.Story ya kutoniswitch off ukilala ikome, kwani we hapo hutaki mie nidoze?!? Unafikiri mi ndo mlinzi wako?!? Narudia tena acha, na mimi nnanmajukumu ya kufikiria usiku.....
5. Saa zingine we huenda na mimi chooni..... Hiyo ni heshima kweli?.....(hata wewe jaribu ku-imagine hata haibu huna unanibofya huku wakata GOoGle?!?! Mi ndo wa kula harufu yako?!?)
6. Mwisho sitaki hiyo tabia umeanza ya off late kunipokea.. Sometimes huwa naliiiiiiiiiiiia muda mrefu haunishugulikii.... Nakupa warning, NITAJIZIMA nisiwake tena!!! Simu yenyewe mchina,HAIBU HUNA kuniliza mbele za watu?!?
7. Nataka uniheshimu kama huyo mjinga mwenzako ambaye ukinywa maji wamuona kwenye glass... Tena acha tabia ya kunitemea mate UKIMKISS kupitia mimi, mambo mengine mfanye mkionana, khaaa!!!
8.Na usisahau kuwa huwa unaniumiza xana wakati umenda kutembea ukiomba omba number, heshimu keypads zangu plz!!!!
9. Tena kuanzia leo nalia bettry low mara moja tu, usipo nicharge nafuta manamba yako yote uliyosave mara KICHECHE ONE, MARA VODA FASTA, MARA WA VIZINGA, oooh, sijui KIDUMU 4.... Acha, TUMIA MAJINA YANAYOTAMBULIWA KISERIKALI!!!!
10. Tabia yako ya kunitumia mimi kutongozea madem zako naomba uiache kwanI mimI sio messenger wako cku nyingne nitazimika kati kati ya maongezi.
11. Mwisho kabisa kama ukigombana na mtu mtafute umtukane live ukimuona sio unantegemea mimi kupitisha matusi yako... Na uchague maneno ya kuongea vinginevyo ntaya- DIVERT POLICE DIRECT kuku weeh!!!!
N.B: Tabia ya kunitumia mimi kama ndo CHAMBO wako wa kuwaambia uko OYSTERBAY kwa Ancle wako, kumbe uko TANDALE KWA MTOGOLE kwa bibi yako naomba uache eeeh!!!!