Belle 9 afunguka kuhusiana na Burger Movie Selfie Remix

By    
Yakiwa yamebaki masaa machache kabla ya kuachia chupa lake jipya la mrudio msanii Belle 9 amefunguka kupitia ukurasa wake wa facebook kuhusu remix ya wimbo wake wa BURGER MOVIE SELFIE ambayo wengi wameipa jina la BMS. 
 Belle 9 aliandika sababu hizo hapo chini;
Jambo la 1: Ni Remix yangu ya kwanza kufanya. Maombi yalikuwa makubwa si kutoka kwa mashabiki tu bali hata wasanii wenzagu ili waweke vionjo vyao.

Jambo la 2: Remix ya BMS inaingia kwenye historia ya kuwa remix ya R&B iliyoshirikisha wasanii wengi kwa pamoja. Nimeshirikisha jumla ya wasanii 5.


Jambo la 3: Remix ya Burger Movie Selfie imeguswa na mikono ya watayarishaji mahiri wanne.

Jambo la 4: Video ya wimbo Burger Movie Selfie Remix imepitia mikono ya waongozaji watatu mahiri.