Mtoto wa Diamond Platnumz afunika kwa kuwa na followers wengi kwenye mtandao wa Instagram

By    


Latiffah aka Tiffah Dangote or princess tiffah  hajamaliza hata siku moja lakini tayari ni staa si tu kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari bali hata kwenye midomo ya watu wanaofuatilia burudani barani Afrika.

Wazazi wake mwenyewe wanamuita ‘The Next Most Famous Daughter in Africa.’ Kwa ukubwa wa Diamondplatnumz na mama yake Zari , hakuna ubishi kuwa Tiffah ana kila sifa ya kuja kuwa ‘binti maarufu zaidi barani Afrika.

Ikiwa ni saa chache tu tangu kuzaliwa kwake, akaunti yake ya Instagram iliyofunguliwa imefikisha followers zaidi ya 25,000.

Picha yake ya kwanza kuwekwa kwenye akaunti hiyo ina zaidi ya comments 1000. “Welcome to the next most famous daughter in Africa… my dad and mom decided to call me Latiffah but I wanna be called Latty or Tiffah #princesstiffa #lattyplatnumz,” yanasomeka maelezo kwenye picha hiyo.

Makadirio ni kuwa akaunti hiyo inaweza kuvuka followers laki moja ndani ya siku mbili au zaidi ya followers 200k hadi wiki inaisha. Hiyo ni speed kubwa sana kwa akaunti ya Instagram kupata followers kiasi hicho.

Mashabiki wa Diamond na Zari na wana shauku kubwa ya kuiona sura ya malaika huyo. Hakuna uwezekano wa wawili hao kuiweka sura yake mapema. Hamu ya watu kutaka kumuona mtoto huyo inaweza kutumiwa kama fursa ya kibiashara na wazazi wake.

Na pengine Diamond na Zari wanaweza kuwa miongoni mwa mastaa wachache wa Afrika (kama wapo) waliowahi kuingiza fedha kupitia picha za mtoto wao. Kipaji cha Diamond na Zari cha kutengeneza fursa za kibiashara kinaweza kuwasaidia kumfanya mtoto wao kuanza kutengeneza fedha akiwa na umri mdogo.

Kufunguliwa akaunti ya Instagram ni hatua ya kwanza katika kumbrand mtoto huyo na kwakuwa mtandao huo umekuwa ukitumika kuwaingiza fedha wasanii duniani, usishangae siku za usoni, makampuni makubwa hasa yanayojihusisha na bidhaa za watoto, yakaichukua akaunti hiyo (retain) ili waitumie kwenye promotion za bidhaa zao. Na isitoshe deals zimeshaanza kuingia.

Umaarufu wa mtoto wa kwanza wa Diamond si kitu ambacho hakikutarajiwa. Habari kuhusu wapenzi hao kumkaribisha duniani mtoto wao kwa siku kadhaa itatengenezwa vichwa vya habari katika bara zima la Afrika.