Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii Bonta amelaani kitendo cha kuipa tuzo video bora ya mwaka ambayo imeongozwa na kufanywa nje ya nchi na kukiita kitendo hicho ni suala la kuua vipaji vya waongozaji wa ndani huku akikifananisha kitendo hicho ni sawa na kuweka dagaa wa kigoma na papa wa baharini mwenye njaa kali katika kapu moja
Hichi ndicho alichofunguka mkali huyo kutoka weusi "KTMA INAUWA VIDEO DIRECTORs WA TANZANIA
ni kawaida kila baada ya Tunzo zozote kunakuwa na mfululizo wa lawama za hapa na pale kuwa flani hakustahili ama flani kaonewa na hii yote inatoka na kuwa HUMAN BEINGS ARE SELFISH IN NATURE so wanaathirika sana na matukio km hayo!!
turudi kwenye mada, nilifatilia kipengele cha VIDEO BORA YA MWAKA na baadhi ya washindanishwaji walikuwa Ay,Diamond,Alikiba ambao video zao wote zimedirectiwa na madirector wa nje ya Tanzania,na iliyoshinda pia ni video ya director wa nje!!nini maana yake sasa unapokusanya madirector wa nje na kuja kuwashindanisha hapa Tz eti unatafuta video bora ya Tanzania!!hapo ni unatafuta video bora ya nje na kuendelea kuwakuza madirector wa nje!! nina hakika ili msanii ashinde video bora mwakani lazma aende nje ndio maana utaskia daily wasanii wetu wapo SA!! ni ukweli usiopingika kuwa madirector wetu bado ni wachanga ukilinganisha na wa nje!!jiulize nani anaetakiwa kuwalinda na kuwakuza???kama taasisi inayoaminika inawatunza waliofanya vizuri mwaka husika inathubutu kuwaweka kwenye pool moja dagaa wa kigoma na wale papa wenye njaa kali wa pwani ya somalia??!!!
kuna kipindi ktk soka vilabu vya hispania na italy viliwekewa kiwango cha kusajili wachezaji wa nje ili kuwalinda wazawa, kiuchumi miaka 25 iliyopita China ilikuwa hairuhusu bidhaa yoyote kutoka nje ili kuvilinda na kuvikuza kwanza viwanda vyake lakini sisi tuliruhusu ndio maana viwanda vya nguo, nyuzi, ngozi, maziwa nk vilikufa!!!
KTMA ilimuuwa Adam Juma na sasa inawauwa Nisher, Hanscana, Khalfani nk"
"