BARNABA BOY, MSHINDI ASIYE NA TUZO WALA KUTAMBULIKA!

By    
Unapoongelea mafanikio ya wasanii kama Linah, Vanessa Mdee au Ruby kimuziki basi huwezi kukosa kumtaja kijana mmoja aitwae BARNABA. Na si hao kunalist kubwa sana ya wasanii ambao nyuma ya mafanikio yao Barnaba kahusika kwa kiasi kikubwa.
KIUKWELI KIJANA HUYU ANAFANYA KAZ KUBWA SANA KIMUZIKI LAKINI KWA MAKUSUDI TUMEAMUA KUTOKITAMBUA  ANACHOKIFANYA.
Barnaba amekuwa akitunga si tu nyimbo zake bali kuwatungia hadi wasanii wenzake, angekuwa USA tungempa jina la GHOSTWRITER.

Lakin kwakuwa lengo lenu ni kuwabeba wasanii fulani kinguvu ili kuwakomoa wasanii wengne, mmeamua kumnyima tuzo yake ya MTUNZI BORA, huku mkijiumbua wenyewe kwa kumpa tuzo kibao msanii anaeandikiwa na huyu jamaa.

Nchini USA ambako tuzo za BET hufanyika, waliwai mpambanisha Diamond na wasanii kama Davido na kiukweli kwa kura tu Diamond alishinda, ila kura sio kigezo cha pekee zinachangia 60% ya ushind, 40% zinazobaki zinaamuliwa na COMMON SENSE ya majaji NDIO MAANA Davido mwisho wa siku alishinda kwa common sense Inayobebwa na kazi halisi.

KTMA mliwai kutuambia miaka kadhaa iliyopita kuwa kura sio kigezo cha pekee kuamua mshindi, JE INAMAANA COMMON SENSE YA MAJAJI WENU NDIO IMEWAONESHA BARNABA hastaili iyo tuzo?

Afu mbona mwaka huu mmekuja kujitetea sana kuusu kura tu, hamuongelei mchango wa majaji???
Atakuwa anajisikiaje kijana wa watu akifikiria mnachomfanyia mashabiki? Unapoongelea mtunzi bora wa wasanii wa kuimba KWA mwaka uliopita basi BARNABA IS THE SECOND TO NONE na sijamuona ata aliyevuka nusu yake.
 
Ikifika 2020 mtapoanza kuuliza imekuwaje Barnaba hana tuzo na ndio mjue blunders mnazifanya sasa makusudi asipate.

Source: MartinFlorian Mgeni