Msanii mwenye jina kubwa Afrika na dunia nzima kutokea kwenye ardhi ya JK azidi kupasua anga na kuwadondosha udenda wasanii wenzake kwa kuweka wazi kazi zake. Sasa anakuja na wimbo mwingine akimshirikisha msanii wa kimataifa Mr. Flavour ambaye ashafanya nyimbo nyingi na kali na wasanii mbali mbali ndani na nje ya Nigeria. Wimbo huo unaenda kwa jina la Nana lakini bado hajaweka wazi kipi kinachozungumziwa ndani ya wimbo huo.
Kama unakumbuka Diamond ashafanya nyimbo nyingi na kali akiwashirikisha wasanii kutoka Nigeria ambazo zimemfikisha mbali sana na kumfanya kuwa nominated katika tuzo mbalimbali kama zile za Chanel O, MTV, AFRIMAMA na nyingine nyingi za hapa nyumbani Tanzania na Afrika.