BIFU YA DIAMOND PLATNUMZ NA Q CHIEF KWISHA, SASA WAAMUA KUFANYA WIMBO WA PAMOJA

By    

Kama ni mfutiliaji mzuri wa muziki na wasanii wetu utakumbuka kuwepo kwa bifu kubwa kati ya Diamond na mkongwe Q Chief baada ya Q kudai kuwa Diamond anatembelea nyota yake (anamloga).
 Good news ni kwamba bif hilo limekwisha na Diamond amempa ofa ya kumlipia Q chief audio pamoja na video ili atusue maana ni msanii ambae anaemkubali.
 "Q Chief namkubali sana, anajua sana kuimba, ana miziki ambayo watanzania wanaipenda sana lakini sifaham tatizo ni nini siwezi kujaji, lakini
sikuzote natamani, kuna kipindi lani nishawahi nilikua nipo na prof jay nakumbuka nilikuwa niko uingereza nikamwambia ukikutana nae zungumza nae mwambie mi ntamlipia video na audio akashoot akafanye ngoma ambayo naamini atatusua, lakini bahati mbaya sijui ikawaje kawaje ikaishia hivyo.Ni mtu ambae natamanigi nisikie ngoma zake kila dakika...." amesema Diamond.