WAJUE WASANII WA TANZANIA WANAOFANYA MZIKI NJE YA TANZANIA

By    
•Kuna wanamuziki wa Tanzania wengi walio nje ya nchi lakini wengi huwa hatupati nafasi ya kuzijua na kuzisikia kazi zao wakiwa ughaibuni.
•Leo tuwatambue wakongwe na nguli wa muziki wa dansi  nchini wakiwa mabalozi wetu nchini Japan wakiwa na kundi linaloitwa Tanzanite Band
•Hawa ni Fresh Jumbe (mwimbaji, katikati), Abbu Omar (Solo Guitar, kulia) na Lister Elia (key board, kushoto).
•Fresh Jumbe amepitia bendi kubwa sana nchini kama Dar International (Super Bomboka), JUWATA Jazz (Msondo Ngoma), DDC Mlimani Park (Sikinde), Orchestra Safari Sound (Ndekule) na Bicco Stars. Kabla ya kwenda Japan alipata pia kuwa nchini Kenya ambako alipiga kwenye bendi kadhaa ikiwemo Angusha Band. Habari za Fresh Jumbe zimeandikwa vizuri kwenye http://bit.ly/1pzbsio. Pia ana mtandao wake wa www.freshjumbe.com. Fresh Jumbe pia kwenyehttp://goo.gl/MK8U7d anaonekana akimpatia zawadi Rais Jakaya Kikwete zawadi ya CD JK alipoenda Japan mwaka 2006.
•Abbu Omar alipotoka UDA Jazz “Super Bayankata” alienda Kenya kushikilia mpini wa rhythm guitar katika bendi ya Simba Wanyika bendi inayoaminika kuwa bendi bora kuliko zote zilizopata kutokea katika historia ya Afrika Mashariki. Alienda kuchukua nafasi ya Omar Shabani aka “Professor” aliyeenda kuanzisha bendi ya Les Wanyika (iliyotunga wimbo wa “Sina Makosa”). Abbu Omar aliyamudu mno mapito ya Omar Shabani kiasi cha kuitwa “Professor Juniour”.
•Lister Elia amepitia makundi mengi nchini ikiwemo Orchestra Safari Sound “Ndekule” na Sambulumaa. Lister Elia ana tovuti yake ya www.listerelia.com.
•Hapa tunauweka wimbo wa “Naima” uliotungwa na Abbu Omar. Wimbo huu utatoka katika album ya " JAMBO AFRICA" chini ya record label ya Tamasha Corporation ya Kenya.

•Wimbo huu umerekodiwa katika studio za Fresh Jumbe zinazoitwa Fresh Studio. Abbu Omar ni mtunzi na amepiga solo. Lister Elia amepiga keyboard. Sehemu ya percussions kama tumba na vinginevyo vimefanywa na Fresh Jumbe ambaye pia ameingiza bass kutokea katika synthesizer. Fresh Jumbe pia ni Sound Engineer.
•Wimbo unaweza kuusikiliza online au kuu-download hapahttp://www.hulkshare.com/un8x0jjw13i8