Juma Mohamed Mchopanga ama kwa jina la kisanii akifahamika kama Jay Moe ni mmoja kati ya wasanii wakongwe hapa Tanzania! Jay Moe ambaye amezaliwa tarehe 27 November ya Mwaka 1978 alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki mwaka 1998.
Jay Moe akiwa ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la Wateule akiwa pamoja na akina Solo Thang, Jafaray, Mchizi Mox na Simba(R.I.P) pamoja na Kelvin ameweza kufanya vizuri na kukonga nyoyo za mashabiki huku wimbo wake uliomtambulisha kama Solo Artist ukiwa "Majukumu".
Jay Moe amekuwa ambaye amekuwa akisfika kwa uhandishi makini na ideas tofauti, majukumu haikuwa mwanzo wa mwisho! Nyimbo kama Bishoo, Mvua na jua na Maisha ya Boarding zilimtangaza vyema katika tansinia ya muziki!
Wengi bado wanaamini "Ulimwengu ndiyo Mama" ya mwaka 2002 ndiyo albamu bora kupata kutokea hapa Tanzania kwa upande wa Hip hop. Ulimwengu ndiyo Mama ilisheheni vibao vingine kama Misosi, Mitungi na Pamba(Ay ), Safari njema(Dudu baya, Complex), Mpenzi kwaheri(TID), Ni mshamba(Sir Nature), Ulimwengu ndiyo mama rmx (Prof j)na Kama unataka demu(Q chief & Solo Thang).
Jay Moe kwa maneno yake mwenyewe anakiri kuwa hakufanya vizuri katika albamu yake ya pili. Hii iliwavunja moyo mashabiki wake wengi mimi nikiwamo. Katika albamu kulikuwa na vibao kama Kasimama peke yake(Banana), Mwingine(Raha P) na Twende kwa mganga!!
Licha ya kutofanya vizuri katika albamu ya pili, Jay Moe hakulala na kukata tamaa, aliendelea kuitumia vizuri mikono ya P.Funk(Bongo Records) na Marco Chali(Kama kawa records). Mawe kama Story 3, Kimya Kimya, Cheza kwa Step(Ngwea), Tingisha(TID), Sihitaji(Lord Eyes) na baadaye Famous(Pfunk) zilizidi kuzihirisha uwezo wake.
Jay Moe akijiita Mchoxx ama Mo-Techniques amekuwa kimbilio la wasanii wengi katika kutaka kuzifanya kazi zao zifanye vizuri, nyimbo kama Jirushe ya Feruz original version haikufanya vizuri kama Remix yake ambamo Jay Moe aliingiza verse yake, vivyo hivyo Nikipata wangu ya K-lyn ilikuja kufanya vizuri baada ya Jay Moe kuingiza sauti yake.
Jay Moe anakiri kuwa na urafiki wa karibu sana TID na umepelekea kufanya kazi kwa pamoja kwa miaka mingi. Kazi walizowahi fanya pamoja ni Zeze, Girfriend, Burudani, Mpenzi kwaheri, Tingisha na kazi ya karibuni kabisa ikiwa inaenda kwa jina la Chumvini!!
Mwisho niseme wasanii aina ya Jay Moe kwa miaka hiyo walijitambulisha kwa ubunifu na kujitengeneza wao kama wao. Kama ni Jay Moe utamsikia Jay moe tu, kama ni Solo thang basi ni Solo Thang tu na Prof J alikuwa ni Prof J peke yake! Ila kwa muziki wa sasa tunawashuhudia akina Stamina wengi tu, akina Young Killer wapo kibao pia, kifupi hakuna ubunifu na ideas tofauti tulizozizoea.