JE WAJUA KWAMBA MBARAKA MWISHEE ALIKUA NI GWIJI WA MUZIKI ALIYEFAHAMIKA SI AFRIKA MASHARIKI TU, NI HADI KATI

By    


Mbaraka mwinyishehe mwaruka alizaliwa mwaka 1944 huko kingowirwa morogoro na alisoma Mzumbe sekondari mwanzoni mwa miaka ya sitini na kuamua kuacha shule na kujiunga na bendi ya morogoro jazz ilikuwa chini ya kulwa salum hadi 1973 alipoanzisha bendi ya super volcano hadi alipofariki tarehe 12/1/1979 huko Mombasa kufuatia ajali ya gari. Cha muhimu ni kwamba marehemu mbaraka alihamia Mombasa Kenya kutokana na ukwasi wa fedha za kununua vyombo vya muziki kufuatia kunyan'gwana vyombo vya muziki na waziri mmoja jina kapuni ambavyo alifadhiliwa na mdau wa nje ya nchi. Pili Mbaraka aliacha historia ya kuwa gwiji aliyejulikana afrika ya mashariki na kati wakati huo. Kwa mfano Franco Luambo makiadi alipokuja TZ mwaka 1973 aliulizwa anamfahamu mwanamuziki gani mashauri TZ alisema ni Mbaraka pekee. Tatu Mbaraka ana historia ya kuwa composer na mpiga solo namba moja ambaye aliweza kupga gitaa la Hawaii (nyuzi 12) ambalo niliwahi kumwona marehemu Ndala kasheba akilipiga. Mwisho Mbaraka alikuwa na kiu ya kutunga nyimbo nyingi zenye maudhui ya mapenzi, matukio ya matukio muhimu yakiwepo ya kitaifa, mafunzo n.k. na bahati mbaya alifariki na umri mdogo wa miaka 35.