MASHAIRI YA STAMINA FT FID Q - WAZO LA LEO

By    

Song: Wazo La Leo
Artist: Stamina Feat Fid Q 
Studio: Bongo Records 
Producer: P funk Majani 
Song Writters: Stamina (verses) & Fid Q (chorus) 

Intro... U know what majani??nice to meet you homie Its moro town baby,,, shorobwenzi 

Verse 1. (Stamina)
Elimika nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo 
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo 
Vaa uaminifu,tupa boksi la kondomu 
Hip hop haijengwi na bifu,underground usijaze fomu 
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe irizi 
Viongozi msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz 
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti 
Mkulima rudi shamba,dec mbegu siku hizi hazioti 
Maisha njia panda,mtembezi chagua pa kwenda 
Uchumi vazi la bwanga,ukishuka uvishe suspenda 
Shiba kwa nia,ukiwa mlafi wa malengo 
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo 
Punguza pupa,mpendaji uingie ndoani 
Mapenzi yamevaa bukta,uswazi mapaja hadharani 
Usilale kijinga,kwenye kitanda cha ushamba 
Unaweza kuwa shabiki wa samba,na ukaishi mwembe yanga

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono 
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono 
Neno la kuponya,lilokosa mdomo 
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo {Hilo ndo wazo la leo}
inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha. {hilo ndo wazo la leo}
usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako- {hilo ndo wazo}

Verse 2. (Stamina)
Underground panga tenzi,ustar hauji kwa promo 
Hakuna tajiri wa mapenzi,kapuku punguza ngono 
Bora uitwe mfalme jua,kwenye utawala wa kishamba 
Mapenzi yakikusumbua, tafuta daktari wa kitanga 
Vazi unaloishi, mwenyezi yeye ndio disegner 
Shetani akikushawishi, mvute kwake kama dayna 
Dunia duara,jitahidi uizunguke 
Mla bata starehe hasara,,wekeza hadhi isishuke 
Huna undugu na bakhersa,niaje aje unakula unga 
Mateja wanahitaji sensa,taifa la kesho linavunda 
Dogo jifunze,heshima sio upaparazi 
Mwambie na dada ajitunze,mlango wake asiuache wazi 
Kama unajijua ni mchoyo,basi usingoje kupewa 
Tafuta pesa kwa moyo,sio kwa ushindi wa ngekewa 
Sharo mpe salamu,the great braza kanumba 
Mwambie bongo sio tamu,na lulu bado wamemfunga 

Chorus(fid q) 
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono 
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo {Hilo ndo wazo la leo}
inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha. {hilo ndo wazo la leo}
usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako- {hilo ndo wazo}

Verse 3. (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi mkasaza 
Nchi tayari imekonda, mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,
kidonda anafanya mtaji ukipata mazuri,
ipange kuikwepa hasara kijana vazi la msuli,
haliwezi kukuvisha busara ukiishi kwa hisia,
kila stone litakubanza cha msingi ni kuweka nia,
ujivue kuwa mtanza kata ya kijiji,
haibebi maji ya maendeleo katibu tunza mkwiji,
msuli ukishuka kimeo uchumi umeshika tama,
kwenye shavu la mlanguzi raia usilaumu chama,
shiriki kwenye uchaguzi unaweza ukavaa kinga,
ila ukafa kwa uaminifu mzinzi usigawe ujinga,
sambaza ujumbe wasifu hakuna snitch kama pesa,
ukiwa nae fanya vya maana akiondoka atakutesa, 
utamsaka usiku na mchana 