STUDIO ANAYOREKODI MZIKI MSANII NEY WA MITEGO YAANZA KUPIGWA ZENGWE

By    









 


Baada ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kuzungumzia mienendo ya wasanii katika tasnia ya muziki na muvi sasa zengwe laanza kuifikia studio ambayo msanii wa bongofleva ambaye nae alikua katika tuhuma mbalimbali zilizotolewa na BASATA juu yake. 
Inasemekana baada ya kutoa ngoma kadhaa ya kuwaponda watu kwa kuwaambia ukweli ulio na maneno makali kiaina, studio anayorekodia Ney wa mitego inayoitwa Shyne Rcords imeandikiwa barua na Basata ya onyo na kupewa siku tano kuonana na basata huku ikituhumiwa kutengeneza ngoma zenye kutukana watu
Mnager wa studio hiyo amesema kuwa michongo hiyo yote itakua imefanywa na maadui wakubwa wa Ney kwenye ngoma zake ambao ni wasanii wa Bongo Movie wametia ndio wamesababisha yote hayo na kuwatuhumu kwa matunguli " yaani sasa hivi unakuta mauza uza tu mara mixer inazima mara amplifaya bila sababu yoyote ila watashindwa tu kwa jina la Yesu." amesema manager huyo..