Muimbaji mkubwa wa Nigeria, D’Banj amemlalamikia Diamond kwa kumzungusha kufanya naye collabo.

Kokomaster amesema kuwa toka walipokutana na Diamond walizungumza na kukubaliana kufanya collabo lakini amekuwa akimpiga chenga mpaka sasa. 
 
Star huyo ambaye aliibuka na tuzo ya ‘MAMA Evolution’ katika MTV MAMA 2015, ameongeza kuwa kabla mwaka huu haujaisha anaamini collabo hiyo itakuwa tayari imefanyika.
Diamond ametoa sababu za kuchelewa kufanya collabo na D’Banj.
 
“Tulikutana kule kwenye Do Agric tukafanya Cocoa na Chocolate, tukatakiwa kufanya nyimbo ya mimi na yeye lakini nikaogopa ukianza na msanii mkubwa sana itakuwa kurudi tena itakuwa tabu lazima uanze kwa ngazi ili kesho na kesho kutwa ukitoa nyimbo uonekane unazidi kupanda, sio unafanya nyimbo na mkubwa halafu kesho unashuka, nafikiri ndio ikawa sababu pia nyimbo yangu ya kwanza sikuweza kufanya na yeye ya kwanza
BAADA mikasa na vituko kibao vya kidume kuchezea kichapo na kuvumilia kitambo huku thamani ya uume ikidhalilishwa front, kijana Nuhu Mziwanda kabwaga mazima, ni Couple iliyounganishwa na yeye na mwanadada mwenye kesi kwa Pilato Basata kwa kumwaga radhi Ughaibu Shilole.

FC baada ya kupata mtonyo iliwaibukia artist hao wenye uwezo wa kuact kila kunapokucha katika kupata data kama ni sinema na wanaendelea na Movie yao mpya ya maisha kama walivyozoeleka? Lakini hii ni real mtu kambwaga mtu naye kaipokea safi.

“Mwanaume umjali mpenzi wake na kumfanyia kile atakacho, lakini si kwa huyu ni mwanamke asiyejua kupendwa na chochote nilichofanya ilikuwa kwa ajili ya upendo tu, nimemwacha na aje mwanaume mwingine naye ajaribu,”Mziwanda

Pia msanii huyo wa muziki amekanusha kuwa kuwepo kwake na mwenye jina la Zuwena Mohamed jina linalofunikwa na hili la ugali la Shilole kuwa hakuwa anamtegemea sana kama ni kwenda Uropa ilikuwa ni mialiko ya kila mmoja kwa dili lake.

FC ilimtafuta mdada makeke awapo kwa stage hadi kusaula viwalo na kuingia matatizoni na wenye mamlaka ya sanaa simu zake zote zilikuwa hazina majibu once mambo yanaendelea, FC imebaini kuwa hakuna watu kubwagana wala nini bali ni mchongo wa machizi hao kutafuta kiki wamepata.

Ilikuwa ngumu kwa wanaomjua Mziwanda eti akijitoe kirahisi hivyo kwa Shilole? Bali wamejipa majina yao ambayo Shilole anaitwa Asha ngedere na Mziwanda jina la Ganda la Ndizi utelezi mwanzo mwisho afanye nini kijana wa watu, maisha ndio yalivyo.

Kumbe walikuwa wanataka Kiki tu, kama Ulaya au wapi hiyo hizi Kiki bhana kuna siku mtu anamua hata Mshua ili mambo yaende. Danganya toto hiyo imebainika baada ya wimbo wao walioshirikiana wasanii hao kuachiwa katika moja ya Redio hivyo hiyo ni movie tu.




Song: Wangu | Artist: Donald & Diamond Platnumz | Director: Justin Campos Share this video on Facebook: http://on.fb.me/1JstLNw Follow me on twitter: @diamondplatnumz
Shilole amesema kuwa Nuh hamwamini kabisaa ana wivu kupitiliza ndio chanzo cha wao kuachana.

"Mimi sina makosa, niko tayari kurudiana nae kama atalijua kosa lake. Kwasasa niko Single nakaribisha maombi”.
Baada mwanamitindo na msanii Jokate kuandika ujumbe mzito kwa Diamond Platnumz na kumshutumu kwa kuweka video inayomuonyesha akicheza wimbo wa “Mdogomdogo” Diamond alipoongea na 255 ya Clouds Fm alimjibu kwa kusema haya.
925673_142672396064017_365086864_n-1024x1024
Diamond amesema “Mimi nimempost kama fan wangu, ile caption yangu sijamuandika jina kwanini achukulie vibaya, ukiona mtu anajishuku ujue kuna namna nyuma, mbona mimi napost watu wengi na caption zangu za vituko vituko manaake mimi nina caption za vituko mi ni mswahili nimezaliwa tandale nimekulia tandale na tandale ndo imenifanya niwe hapa nilipo, kuna caption zangu za uswahili coz uswahili ndio umenikuza mpaka kuwa fame, mbona naandikaga kwenye caption kwann kwake yeye ndo tatizo kwani kuna ubaya gani kuandika mtanyooka tu kama haimuusu,maana ukiona hivyo ujue kuna kitu kinamuhusu, yeye mpaka nimeenda kuchukua tuzo amesapoti nini, alipost hata post moja ya kusema mpigie kura Diamond, anajishaua eti nimesapoti kasapoti nini.”


platnumzzz
Shukran Kubwa sana Zimfikie Mwenyez Mungu kwa Tuzo hii, na pia Shukran za Dhati Ziwafikie Wadau, Media, Wasanii na Mashabiki zangu wote kwa kunipigia kura na Kuhamasisha kwa Nguvu…Niushkuru sana Uongozi wangu, Familia pamoja na Team nzima ya @wcb_wasafi hususan Madancers wangu kwani Naamini wao ndio wamenipika nikapikika hadi leo hii kuweza kuletaTunzo hii Nzito ya Mtumbwizaji Bora Africa, Nyumbani…lakini pia Shukrani za kipekee zimfikie Mama yangu kipenzi Sandra kwa Mafunzo na Malezi anayonipa kila siku juu ya Dunia….na Shukran tena za kipekee na aina yake zimfikie Roho yangu, Kipenzi Changu @zarithebosslady Kwa raha na Usingizi mwanana anipatiao na kunifanya nizidi kutunga na kuwa M’bunifu kwenye kazi.. #BestLiveAct #Mtvmama2015 Asanteni sana
Ilisemekana kuwa Davido na Diamond wana Beef, Lakini Diamond na Davido bado wanazidi kudhihirisha kuwa hakuna Beef kati yao!
Davido na Diamond Platnumz wamekutana nchini south Afrika ambapo wako katika maandalizi ya Tuzo za MTV ambazo zitafanyika Jumamosi hii nchini South Afrika.
 
Hii ni picha ambayo kwa siku ya leo imemake headlines sana katika mtandao wa kijamii wa facebook kutokana na TBT yake kuwa ya muhimu sana na ya fundisho kubwa sana kwa vijana wa kitanzania kwa kuangalia hatua ambazo watu hao katika picha wamepitia na mahali walipo kwa sasa.

 
Akiwa nchini Afrika kusini msanii machachari sukari ya warembo, raisi wa WASAFI amepata nafasi ya kukutana na wasanii wengine wa hapa Afrika na kutoka mabara mengine ambao wako nchini Afrika ya Kusini kwa ajili ya kushuhudia na kutumbuiza katika tuzo za muziki za MTV ambazo Diamond pia ni mmoja ya washiriki. Baada ya kupiga stori na D Banj ndipo Diamond alipopewa taarifa ya kuwa anatafutwa na msanii NE-YO kutoka nchini marekani na kufanikisha kuonana nae na kupiga stori kadhaa ambazo bado hajaziweka wazi kuwa ni kipi hasa ambacho wakali hao wawili walikuwa wakiteta.
LOL! Kumbe suala la kuolewa Ray C alikuwa anajaribisha tu kuona kama mashabiki wake mpo.

"Hapana sina mpango wa kuolewa, mme mwema anatoka kwa Mungu, huwezi sema unatangaza. Sasa hivi sipo kwenye mahusiano sina mtu, nikimpata mtasikia. Kuhusu kutafuta mme wa kunioa huo ulikuwa utani tu, nilikuwa nataka kuwafurahisha watu wangu wa insta. Nimepokea simu nyingi zaidi ya 500 hadi saa 6 usiku. Kwahiyo nimeona mashabiki bado wapo na wananipenda. amesema Ray C
Akilinganishwa na rapa kutoka South Afrika, Nigeria, Ghana na wengine kibao boa wa Afrika, Fid amesema
"Naamini tutafika namba 1 baada ya kuachia hivi vichupa (video) ambazo zipo kwenye ratiba zinazofata, sote kwa pamoja tuseme Amen."
Je unamkubali Fid Q kama rapa bora Tanzania?
Jiunge na marapper wengine kwenye kipindi cha Rush Hour, Ijumaa saa 19:00usiku kwenye MTV Base (DStv 322).
 
July 5, 1982 Ambwene Yessayah alizaliwa. Namshukuru Mungu kwa kuiona siku hii ya leo. Nawashukuru wazazi wangu kwa kunileta duniani. Mungu awalaze mahali pema peponi. Natamani mama yangu angekuwa hai aone jinsi kijana wake alivyokuwa mkubwa na pengine afurahie jasho lake la kunizaa, kunilea na kunitunza.
Nawashukuru wote walio na mchango mkubwa kwenye maisha yangu, ni wengi siwezi kuwamaliza kuwataja. Navikushukuru vyombo vya habari vyote kwa support kubwa inayoendelea kunipa. Nakushukuru pia wewe shabiki yangu kwa kuendelea kuniunga mkono. Thank You!!
Hit Maker wa single ya Nakumis Timbulo ameachia Single yake Mpya aliyoipa jina la Yupo iko hapa chini Download 


Baada ya kuonekana kwa muda kidogo kwenye media kutokana na mahaba niue na mdada Shamfa Ford kutoka Bongo movie kwa kile kilichodaiwa kuwa wawili hao ni wapenzi, Nay awajibu na kuwaambia mashabiki kuwa hana muda. Sikiliza na pakua nyimbo hiyo hapo chini

 
Poleni marafiki mlio sikitishwa na tukiwa langu la kupokonywa mtoto- nimeona mnahitaji kujua ili muache masikitiko na tufurahie wakati uliopo- ni Kweli baba yake alishinda KESI lkn sheria hairuhusu nazani alitumia rushwa au labda cheo chake maana haijulikani alishindaje - any way nataka tu mjue mtoto wangu ninae na mimi si mwanamke regerege wa kupokonywa haki zangu za kumlea mwanangu ! Nimekwenda kwenye vyombo vya sheria na vinafanya kazi na. Niwahikikishie tu ntashinda kwa kuwa nina haki na ni mama bora- nitasimama mpaka kieleweke bila kujali cheo wala pesa - sheria zimewekwa na haki zinatendeka- mpaka sasa niko vizuri tu- niko na sasha na ntaendelea kuwa nae mpaka umri utakapo ruhusu lkn si leo wala kesho hayo ya mbele mungu ndio anayajua.....na niwaambie tu wale watoa hukumu wa humu ndani- KATIKA SHERIA YA TANZANIA NA DUNIANI HAKUNA KIPENGELE KINACHO MFANYA MAMA APOKONYWE MTOTO KUPITIA MAVAZI- KUNA VITU VYA KUZINGATIA VYA MUHIMU LKN SI MAVAZI!
Source: Joyce Kiria (Facebook)

 
Star wa muziki Barnaba, amejinadi kuwa albamu yake mpya itaingia sokoni kwa bei ya dola 100 ama zaidi, pesa ambazo zinakadiriwa kufikia shilingi laki 2 za Tanzania kwa nakala 1.Mkali huyo amekuwa akijiamini kutokana na ubora wa nyimbo, utofauti na uwekezaji mkubwa anaoendelea kuufanya kukamilisha kazi hiyo.Barnaba ameeleza kuwa, baadhi ya rekodi kutoka albam hizo zimekwishapelekwa nchi mbalimbali ikiwepo Afrika Kusini na Ujerumani kwaajili ya 'Mastering', zikitarajiwa kutoka kwa mfumo wa DVD, na vile vile CD za kawaida, kwa bei hiyo ambayo hata hivyo amesisitiza kuwa inaweza kuongezeka zaidi.

Source: EATV
Star wa nchini Uganda, Bebe Cool ameendelea kushikilia msimamo kuwa, kwa upande wake staa wa muziki Eddy Kenzo ni msanii anayechipukia, licha ya mafanikio ya kitaifa na kimataifa ambayo Kenzo ameendelea kuyapata kupitia kazi zake.
Source EATV