Umoja wa wasanii wa muziki wa bongo flava kutoka jijini Dodoma wameachia audio ya wimbo wa maombolezo baada ya kutokwa na msanii wa kundi la Chamber Squad, Mez B. Wimbo unaitwa R.I.P Mez B
kidawa izzo b
Nyota wa muziki wa rap nchini Tanzania, Izzo Bizness ameachia audio ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Kidawa’ aliomshirikisha mwanadada Sarah Kaisi ‘Shaa’ uliofanyika ndani ya studio za Uprise Music chini ya mtayarishaji mahiri nchini Duppy na kufanyiwa mastering na Master J wa MJ Records. Usikilize hapa……

Katika jitihada za kupambana na matukio ya kinyama ya Mauaji ya Albino nchini, Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiongozwa na Keisha wametengeneza rekodi maalum kusaidia kuongeza uelewa na kukemea ukatili huu dhidi ya walemavu wa ngozi.


Kuhusiana na Project hii, inayokwenda kwa jina la Simama Nami, eNewz ya EATV imeongea na Keisha ambaye kwa hisia nzito amefafanua maana ya rekodi hiyo na kuwataka watanzania kila mmoja kwa nafasi yake kusimama na kupambana dhidi ya vitendo hivyo vya kinyama vya mauaji ya albino.
KEISHA.
Keisha amesema kuwa, imamuuma sana na anakata tamaa na nchi yake kila siku zinavyozidi kwenda. “Natamani niiikimbie hii nchi niende mbali ambapo labda sitoweza kushuhudia huu ukatili unaoendelea ndani ya nchi mnayoiita nchi yenye amani.”


Msanii anayetikisa kwa mziki mzuri na tuzo nyingi zaidi nchini Tanzania kutoka WCB atoa shukrani zake kwa watu kibao akiwemo Mh. Waziri Membe kupitia akaunti ya facebook. Huu ndio ulikuwa ujumbe wake mfupi wenye maneno mazito kwa watu hao.

Eeh Mwenyez Mungu Nakushkuru sana kwa kuweza kunipa ujasili na Moyo wa kuyavumilia yote niliyo yapitia... Asante sana Mh Benard Membe, Joseph Kusaga, Haroun na Kampuni Nzima ya Spice, Mh . Nchimbi, Dk Dossaj , Uongozi wangu, jamaa na Marafiki, Mashabiki zangu pamoja na Familia yangu pendwa kwa kuwa nami bega kwa bega katika kipindi chote cha Miezi hii Miwili Migumu kwangu....Nawashkuru sana

TIMU NZIMA YA SIKILIZA MDUNDO BLOG INAPENDA KUKUPA POLE SANA PLATNUMZ KWA MAGUMU ULIYOYAPITIA NA HASA KUUGULIWA  KWA MAMA YETU MPENDWA, MUNGU AKUPE WEPESI.
SIFA ZA MWANAUME AMTAKAE LADY JAYDEE KWA SASA
Mwanaume mwenye vigezo gani ungependa kuwa nae kwa sasa?

JIBU :Anaejali na kuheshimu, mwenye roho ya upendo na huruma, anaeweza ku take care of me financially.Asiechepuka hovyo (Milupo kila kona ),Asiwe tegemezi.Hata kama sio tajiri lakini asinitegemee.Asiwe mlevi kupindukia wa kulala bar,Wala kulala nje kwa machangu wa Kinondoni au popote pale.Nikikohoa tu awepo hapo
Msanii wa Bongo movie aamua kutoa yaliyo moyoni kupitia mtandao wa kijamii wa IG. Hiki ndicho alichokiandika

"Morning my people..samahani kama nitakuwa nawakwaza but sometimes ni bora kutoa dukuduku lako..To be honest huwa wananiboa wale wa R.I.P WA INSTA...inaeleweka kwamba kutokana na majukumu ya kimaisha si kila kitu utaudhulia.sometimes inaweza ikatokea msiba labda umesafiri au unaumwa au dhalula yoyote inaeleweka

But hawa wenzangu na mimi msiba unatokea utaona R.I.P kubwa na kwenye msiba haendi..na si kwamba kabanwa wala,maana baadaye mnaweza kutana viwanja.isingekuwepo INSTA je.? Weka R.I.P na kama hujabanwa nenda msibani.nawajua hawa maana insta ataweka hadi vialama vya kulia but msibani halitokei ila usiku unakutana nalo club."



Kundi la Muziki wa Kizazi kipya Yamoto Band wanatarajia kuanza safari yao ya kwenda UK kufanya Show tarehe 17 mwezi huu na show itapigwa Tarehe 21 ndani ya Royal Regency.


Mkurugezi wa Kundi hilo Mkubwa Fella kwanza alianza kwa kutoa shukran zake kwa Mwenyezi Mungu, Mashabiki, Wadu na vyombo vyote vya habari kwakuweza kutoa sapoti kwa vijana hao tangu walipo toa Kazi yao ya kwanza kabisa mpaka kufikia Leo wamepata mualiko mkubwa kabisa wa kwenda kufanya show UK, na kwa upande wa Msemaji mkuu na Kiongozi wa Band Aslay Isihaka amesema kuwa wanafuraha sana kwa kupata mualiko huo lakini pia wanashukuru kwa mungu, mashabiki na wale wote wanaonyesha sapoti katika muziki wao. Aslay amesema kuwa watakwenda kufanya Kazi nzuri huko ili kuleta sifa ya muziki wa hapa nyumbani na hata heshima ya Taifa kwa ujumla.Kwa upande mwingine Vijana hao Wametoa shukrani zao kwa Viongozi wao Mkubwa Fella, Bab Tale, Chambuso, Mh Temba na Shirko kwa usimamizi Mzuri wa Kazi hizo.
Baada ya "SISIKII" Kufanya vizuri Audio na Video sasa kwa mara nyengine tena Jux anawaletea wimbo mwengine mpya ambao ameutambulisha kwa jina la "NIKUITE NANI?".


Baada ya kutoa mixtape inayoitwa   Sorry 4 The Wait 2  rapa huyo mwenye mgogoro mkubwa na Birdman na Cash Money.

Lil wayne kupitia akaunti yake ya mtandao wa twitter (@LilTunechi) ametangaza kutoa album ya bure The Free Weezy Album  kwa mashabiki wake kwa kuwa na uvumilivu wa kuisubiri albuma yake mpya THA CARTER V ambayo bado Cash Money na Universal  hawajaiachia. 





Kama ulikuwa umeyakosa yale mahojiano na Muheshimiwa Tundu Lissu kwenye Mkasi Tv basi usipoteze muda bofya play hapo chini ujionee mwenyewe