R.I.P Mangwea

Bingwa mtetezi wa michuano ya French Open Serena Williams ametolewa katika michuano hiyo na Gabine Muguruza kutoka Spain katika siku ya nne. Mapema dada yake Serena, Venus, alitolewa na Anna Schmiedlova kutoka Slovakia. Hii ni mara ya kwanza kwa Serena kushindwa kuingia katika wiki ya pili ya michuano mikubwa kama mchezaji wa juu. Matumaini ya dada hawa wawili kukutana katika raundi ya tatu sasa hayapo, na itakuwa kati ya Muguruza na Schmiedlova
Ni video teaser ya wimbo unaotikisa katika katika anga la Bongofleva katika radio stations zote Tanzania na nje ya Tanzania. Hivi punde siku chache zijazo video hiyo itakuwa hewani kwani kila kitu kiko sana kabisa kilichobaki ni kuiingiza sokoni tu. 
SI YA KUIKOSA, MWAMBIE NA MWENZIO, USISUBIRI KUJUA UZURI WAKE.



Juma Mohamed Mchopanga ama kwa jina la kisanii akifahamika kama Jay Moe ni mmoja kati ya wasanii wakongwe hapa Tanzania! Jay Moe ambaye amezaliwa tarehe 27 November ya Mwaka 1978 alianza rasmi kujishughulisha na kazi ya muziki mwaka 1998.

Jay Moe akiwa ni mmoja wa waanzilishi wa kundi la Wateule akiwa pamoja na akina Solo Thang, Jafaray, Mchizi Mox na Simba(R.I.P) pamoja na Kelvin ameweza kufanya vizuri na kukonga nyoyo za mashabiki huku wimbo wake uliomtambulisha kama Solo Artist ukiwa "Majukumu".

Jay Moe amekuwa ambaye amekuwa akisfika kwa uhandishi makini na ideas tofauti, majukumu haikuwa mwanzo wa mwisho! Nyimbo kama Bishoo, Mvua na jua na Maisha ya Boarding zilimtangaza vyema katika tansinia ya muziki! 

Photo
Wengi bado wanaamini "Ulimwengu ndiyo Mama" ya mwaka 2002 ndiyo albamu bora kupata kutokea hapa Tanzania kwa upande wa Hip hop. Ulimwengu ndiyo Mama ilisheheni vibao vingine kama Misosi, Mitungi na Pamba(Ay ), Safari njema(Dudu baya, Complex), Mpenzi kwaheri(TID), Ni mshamba(Sir Nature), Ulimwengu ndiyo mama rmx (Prof j)na Kama unataka demu(Q chief & Solo Thang).

Jay Moe kwa maneno yake mwenyewe anakiri kuwa hakufanya vizuri katika albamu yake ya pili. Hii iliwavunja moyo mashabiki wake wengi mimi nikiwamo. Katika albamu kulikuwa na vibao kama Kasimama peke yake(Banana), Mwingine(Raha P) na Twende kwa mganga!!

Licha ya kutofanya vizuri katika albamu ya pili, Jay Moe hakulala na kukata tamaa, aliendelea kuitumia vizuri mikono ya P.Funk(Bongo Records) na Marco Chali(Kama kawa records). Mawe kama Story 3, Kimya Kimya, Cheza kwa Step(Ngwea), Tingisha(TID), Sihitaji(Lord Eyes) na baadaye Famous(Pfunk) zilizidi kuzihirisha uwezo wake.
Jay Moe akijiita Mchoxx ama Mo-Techniques amekuwa kimbilio la wasanii wengi katika kutaka kuzifanya kazi zao zifanye vizuri, nyimbo kama Jirushe ya Feruz original version haikufanya vizuri kama Remix yake ambamo Jay Moe aliingiza verse yake, vivyo hivyo Nikipata wangu ya K-lyn ilikuja kufanya vizuri baada ya Jay Moe kuingiza sauti yake.

Jay Moe anakiri kuwa na urafiki wa karibu sana TID na umepelekea kufanya kazi kwa pamoja kwa miaka mingi. Kazi walizowahi fanya pamoja ni Zeze, Girfriend, Burudani, Mpenzi kwaheri, Tingisha na kazi ya karibuni kabisa ikiwa inaenda kwa jina la Chumvini!!
Mwisho niseme wasanii aina ya Jay Moe kwa miaka hiyo walijitambulisha kwa ubunifu na kujitengeneza wao kama wao. Kama ni Jay Moe utamsikia Jay moe tu, kama ni Solo thang basi ni Solo Thang tu na Prof J alikuwa ni Prof J peke yake! Ila kwa muziki wa sasa tunawashuhudia akina Stamina wengi tu, akina Young Killer wapo kibao pia, kifupi hakuna ubunifu na ideas tofauti tulizozizoea.
Cristiano Ronaldo and Irina Shayk
COVER PHOTO YA VOGUE LINALOTARAJIWA KUINGIA MTAANI VERY SOON

View image on Twitter
RONALDO AKICHEZEA MPIRA NA SUTI YAKE, HUKU IRINA AKIWA AMEPOZI PEMBENI TAYARI KWA KWENDA MAZOEZI.
SHUKA NAZO...
Mwasiti
Serebuka
Dir: Nick Dizzo

p1

Ikiwa ni mfululizo wa wasanii kibao kubadili mitindo yao ya nywele siku hadi siku, sasa ni zamu ya msanii marufu kutoka kundi la P Square kutoka jijini Lagos Nigeria.

Peter Okoye aamua kubadili mwonekano wake kwa kuamua kunyoa nywele zake. Amini usiamini as a good father na mfano wa kuigwa kapendeza sana kwa mtindo huu mpya kitu kilichowavutia mashabiki wengi sana wa kaka huyu kutoka kundi la P Square,
p2

Mwonekano huu umeonekana kuwapendeza wengi ikiwemo ni Starboy Wizkid ambaye aliandika kupitia mtandao wake wa 212, nanukuu Nice haircut and s*xy body""

p3

IMG-20140513-WA00001
Wimbo Mpya: Nick wa Pili feat G-Nako &Ben Pol -Staki Kazi

Baada ya kukwapua tuzo saba katika tuzo za KTML 2014,Diamond aamua kuwaonesha mashabiki wake kwamba hakubaatisha na bado uwezo anao....
hii ni demo ya wimbo wake huo mpya ambao utatambulishwa rasmi wiki ya kesho, Sikiliza na Download hapa=>http://www.hulkshare.com/626w3d9uiolc
n1
Mwanadada mwenye makalio makubwa na umbo na kuvutia kama wengi wamwitavo 'Bust Baby', Nicki Minaj aonyesha umbo lake katika vinguo viwili vya Norma Kamali swimsuit na viatu virefu vya Gucci  akiwa katika pozi la kurekodi tangazo la Myx Fusions Moscato. Picha zaidi zicheki chini;
P-Square drops yet another breathtaking visuals for their newest smash hit single "Taste the Money" (Testimony). The twin boys are really enjoying the pleasures of hard work. Shot in South Africa and directed by Jude Engees Okoye.
Mwana Fa akiwa na wamasai wake usiku wa Kili Tanzania Music Awards
Hii ndo ngoma ambayo Mwana Fa aliitambulisha Exclusive na Kuiperform katika usiku wa utoaji wa Tuzo za Kili Tanzania Music Awards iliyofanyika katika ukumi wa Mlimani City, watu walikua wanaiskia kwa mara ya kwanza lakini vibe yake ilikua kali hii ina maanisha kuwa ngoma tayari ni Hit tangu siku ya kwanza, Fa aliperform na watu kibao waliokua wamevalia shuka ama nguo za kimasai waliokua wanaruka ruka on stage, enjoy dude hilo hapo chini
Kwa mara ya kwanza mkali wa HIP HOP anayekubalika sana bongo apata tuzo za Kili mbili. Fid Q amekiri kwamba tangu mwaka 2000 hadi mwaka jana hakuwahi pata tuzo hizo pamoja na kupendekezwa kwa miaka hiyo kumi yote. 

Fid amesema kuwa kwa miaka mitatu iliyopita hajahudhuria tuzo hizi na amekuwa akiomba mtu akamwakilizhe lakini hawakurudi na tuzo na kwa mwaka huu aliamua mwenyewe kuhudhuria ili ashuhudie mwenyewe na amekiri kuwa asingepata alishapanga kwamba ni ilikuwa ni mara yake ya mwisho kuhudhuria. Lakini safari yake hiyo imekatishwa na tuzo hizo mbili alizojinyakulia bila kutegemea.

Hapa alipanda jukwaani na Mwana FA na kumuomba azungumze kitu na ndipo FA alipotoa ahadi ya kufanya ngoma ya pamoja na Fid Q siku ya kesho, so lets wait for a new joint between Fid and FA.
Fid akiwa na Tuzo yake mkononi
Ushindi wa Fid umeonyesha kuwafurahisha wengi na kuwapa tumaini la kuendelea kuwa na matumaini na KTMAkwani zimekuwa ni tuzo zinazopewa lawama sana na wasanii na mashabiki wengi na kuonekana kuwa ni tuzo za upendeleo. Furaha hiyo pia imeonyeshwa na msanii Ommy Dimpoz na mashabiki wengi kupitia mitandao ya kijamii kwani Fid amekuwa ndio habari ya mujini kwa sasa.
Zikiwa zimebaki wiki mbili kuachia wimbo wake mpya kwa ajili ya album yake ya tatu The Pink Print mwanadada mwenye vituko na mvuto ambaye yuko chini ya label ya mtu mzima Bird Man, Young Money aamua kuachia mziki mpya kabisa ambao kamshirikisha mtu mzima Soulja Boy ukienda kwa jina la Yass Bish. Ucheki na download hapo chini
Yasss Bish!








"NISHIKE", third single off Sauti Sol's upcoming third album. Song written and performed by Sauti Sol.
Produced by Kagwe Mungai.
Video directed by Enos Olik/Bokeh Family 2014.
Assistant Director: Marvine Obaga.
Video Styling: Anabelle Onyango.
Executive Production: Sauti Sol Entertainment.
Nishike (Swahili for Touch Me).
Follow @SautiSol
Moja ya kitu kizuri katika maisha ya mwanadamu ni kuona unapata mafanikio kwa juhudi ulizoziweka katika mambo mbalimbali. Mwanamuziki Hamis K kutoka Moro town, mkoa wenye vipaji vya muziki vingi amekuwa ni kati ya vijana wenye juhudi kubwa na makini katika kazi zake kitu kilichoweza kuwashawishi Abood TV kuweza kumchukua Hamis K kuwa one of the host wa kipindi cha STAR KONA kinachofanya interview na wasanii mbalimbali.

Hii ni picha aliyopost kupitia ukurasa wake wa facebook na kuachia caption hii "Ni moja ya show nnazo host nikiwa na anna, inaitwa STAR KONA inayorushwa na abood tv ! interview hii ilikuwa nguuuumu coz nilikua nawahoji wasanii wa comedy KINYAMBE na MDANANDA yaaaani walikuwa wanatuuchekesha balaa yaaani dah ila tumemaliza pouwa. kwa wale wakazi wa morogoro keep on watching ATV"

Mbali na Muziki kwa sasa Hamis ni mwanafunzi wa chuo kikuu na ni prodyuza wa muziki wake mwenyewe akifanya kazi zake chini ya studio ya ICON RECORD TZ iliyopo Morogoro maeneo ya maghorofani Kihonda.
The huge collaboration by South African super-group, Mafikizolo, and Nigerian sensation Davido -- courtesy of Twenty Twenty Media -- The song titled "Tchelete (Goodlife)" is produced by Shizzi & Oskido
NI NGOMA AMBAYO IMEKUWA IKISUBIRIWA KWA HAMU SANA NA MASHABIKI WA MUZIKI WA BONGO FLEVA KUTOKANA NA UMAHIRI NA UKALI WA MASHAIRI AMBAO WEUSI KWA UJUMLA WAMEKUA WAKIFANYA. BASI KIU YAKO SANA IMEFIKA TAMATI KWANI MZIGO NDO HUOOOO KWA VIDEO.
KAMA UNACHUKI BASI VAA MIWANI USIONE GERE