Mac Mc (Publik_Figure)_Kitengo Maalum_Feat_G NAKO & Chalii Mtoto wa Bibi (Jambo Squad)
Produced by: Chipa Magneto & John B
Studio: Grandmaster Arusha 






The video is Directed and visualized by Nicklass Mmbaga under iMAGE NATION..
Music is writen and produced by Kaduma
JAMES Dandu ‘Mtoto wa Dandu’ siyo jina geni katika gemu la Bongo Fleva lakini ni wangapi wanamkumbuka na wanautambua mchango wake katika gemu la Bongo Fleva? Ungana nami ili kumjua kwa kina.
James Dandu ‘Mtoto wa Dandu’ (kushoto katika picha) enzi za uhai wake.

HISTORIA YAKE KWA UFUPI
James Dandu au kwa jina lingine Cool James Massive ‘CJ Massive’ alizaliwa Julai 5, 1970, Mwanza nchini Tanzania. Alisoma shule ya Msingi Kurasini na baada ya hapo, yeye, mama yake na ndugu zake walihamia jijini Stockholm, Sweden alikoishi kwa kipindi kirefu.
ALIVYOINGIA KWENYE GEMU
James Dandu aliingia rasmi kwenye sanaa ya muziki mwaka 1988 akiwa jijini Stockholm ambapo alitoa singo kadhaa zikiwa katika staili ya Euro-House. Mwaka 1992 aliachia albamu yake ya kwanza ambayo hata hivyo haikupata mafanikio makubwa.
Mwaka 1993, aliungana na msanii mwingine kutoka Afrika Mashariki, Andrew Muturi na kuunda kundi lililokwenda kwa jina la Swahili Nation. Wasanii wengine wawili wakajiunga kwenye kundi hilo.
Baadaye, James Dandu alijitoa kwenye kundi hilo na kuungana na Mkongomani, Jose Masena ‘Black Teacher’ na kutoa albamu mbili zilizowatambulisha vyema sehemu mbalimbali; Undercover Lover (1992) na Zooming You (1995) iliyokuwa na wimbo ulioitwa Dr. Feel Good. Wakapata mafanikio makubwa na kuingiza mkwanja wa maana.
AREJEA BONGO KWA KISHINDO
Kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata akiwa na mwenzake, Black Teacher, Mtoto wa Dandu aliamua kurudisha majeshi nyumbani kwa lengo la kuja kuibua na kuinua vipaji Tanzania na Afrika Mashariki kwa jumla.
Aliporudi Bongo, alikuja na staili mpya ya uimbaji wa nyimbo za taratibu (R&B) ambao haukuwa umezoeleka sana kwa kipindi hicho. Akajipatia umaarufu mkubwa ndani ya kipindi kifupi.
Hakuishia hapo, aliendelea kuingiza ubunifu katika kazi zake, akawa anachanganya R&B ya kisasa, Rhumba na Ndombolo (staili iliyokuwa maarufu sana nchini Zaire kipindi hicho). Akatoa albamu nyingine kama Soft Like a Pillow (1997), Bi Harusi (1998) na Sukuma Land (2002).
Miongoni mwa ngoma ambazo mpaka leo zikipigwa lazima watu watulie ni Sina Makosa ambayo aliurudia wimbo wenye jina hilohilo uliopigwa na Les Wanyika kutoka Kenya. Ngoma hii ilimtambulisha kinoma Afrika Mashariki yote, hususan nchini Kenya.
Pia alifanya remix ya wimbo wa Mamu akiwa na mkali Madilu System ambao ama kwa hakika ulibamba mbaya!
TUZO ZA KILI
Mwaka 1999, James Dandu aliamua kuanzisha tuzo alizoziita Tanzania Music Awards ambazo hivi sasa zinajulikana kama Kili Music Awards baada ya kuanza kudhaminiwa na bia ya Kilimanjaro. 
James Dandu ndiye aliyefanikisha usajili wa tuzo hizo kwa kushirikiana na Basata chini ya Wizara ya Elimu na Utamaduni (kipindi hicho).
KIFO CHAKE
Mtoto wa Dandu alifariki Agosti 27, 2002, kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Makumbusho jijini Dar es Salaam, nyota yake ikiwa inang’ara kinoma na kuzusha simanzi kubwa miongoni mwa mashabiki wake, hususan wanawake ambao walikuwa mashabiki wake wakubwa.
Akaenda kuzikwa nyumbani kwao, Mwanza. Wakati anakufa, alikuwa bado hajamaliza kurekodi kazi zake mpya katika Studio ya Master Jay. Aliacha watoto wawili wakiwa bado wadogo pamoja na mjane, Devotha.
MIAKA 12 BAADA YA KIFO CHAKE
Ni miaka 12 sasa imepita tangu Mtoto wa Dandu aliporejea kwenye makazi yake ya milele. Swali ambalo mimi na wewe tunapaswa kujiuliza, je, anapewa heshima anayostahili hata kama alishatangulia mbele za haki? Familia yake wakiwemo wanaye Caroline-Jamie ’Malaika’ aliyezaliwa mwaka 1994 na Michael James Junior aliyezaliwa 1997 wananufaika na matunda ya kazi za baba yao? Nawashauri waandaaji wa Tuzo za Kili wamuenzi James Dandu japo kwa tuzo ya heshima!

Siku ya Ijumaa kuna habari zilivuma kwamba wawili hao wanataka kutengana kutoka mahali wanapoishi, lakini kwa habari kutoka kwa msemaji wao Bayo Adetu zilizolripotiwa na chanzo kimoja cha mjini Lagos amekanusha uvumi huo.
Lakini mtu mwingine wa karibu wa wawili hao amenukuliwa akisema haya


“Yes they fought this week. Peter even left a mark on Paul’s left eye. But the fight wasn’t during rehearsal, which rehearsal? Peter has refused to do anything P-Square for weeks now. Forget that he was at his brother’s wedding, things are not good between them right now. Peter wants out. He said Paul and Jude are sidelining him. That if they push out 200 songs, 199 would be songs Paul did. That people are now calling him a dancer in P-Square. Peter is really angry. He’s even the cool and friendly one between the brothers but he is not himself right now. And then he accused his brother Jude of disrespecting his wife. Peter and Jude haven’t spoken in weeks. Peter said Jude has been disrespecting Lola for years and he was done tolerating the BS. In fact Peter said that not only is Lola older than Jude, but that she’s also pregnant and Jude was upsetting a pregnant woman. If you notice Jude didn’t attend their wedding last year despite the fact that he was in Nigeria. Jude asked Peter why he didn’t marry Lola when their mother was alive. Jude said it’s his wife that is pushing him and they will need to pray for him. In fact nobody in the Okoye family likes Lola and they didn’t support the marriage. The brothers are really angry at each other. The police is even involved. This week, either the commissioner of police or someone from his office visited their house.

The worst part is that they have invited lawyer to come and share property o. They want to share everything. The lawyer was at their house I think on Thursday. Peter said no more P-Square joint ventures. You know they own everything together, including a house in Omole, Parkview and Atlanta. Except something is done fast P-Square is about to be finished. But I know that people have been intervening and begging them to reconsider, that they are the biggest musical duo in Africa. Nobody will benefit if they split. The power to make money is in their togetherness.

It is Jude people are begging to keep the brothers together, but after what he tweeted yesterday, it may truly be over for P-Square. Jude has really tried for his brothers, for him to give up may mean it’s over for them.

He practically put his entire life on hold for his brothers. Even sold his first car to shoot their first video but all that is about to come to an end like he tweeted. The only thing that can save the situation is if by a miracle Jude and Lola settle their differences but I don’t see that happening”




Unapozungumzia mastaa wenye mvuto na maumbo ya kuwafanya wanaume wengi wapagawe basi unakuwa hujakosea ukimtaja mwanadada Selena Williams anayetikisa katika ulimwengu wa tenis. Hizi ni baadhi tu ya picha za Selena akiwa katika vazi la bikini ufukweni huko Miami.




Tafadhari bonyeza link hiyo chini kumpigia kura Diamond Katika tunzo za MTV Africa Mama's Awards kama Msanii bora wa kiume

Na hii, kwa kuipigia kura Number one Remix alomshirikisha Davido kama nyimbo bora ya kushirikiana


Kulia (anayeongea kwenye simu) ni Rama wa Kitaa na kushoto mwenye tabasamu kali ni Hamis K, msanii mwenye ngoma kazaa kali zinazobamba kwenye radio stations na television mbalimbali. Ukizungumzia ngoma ya Kombolela basi utakuwa hujamsahau Hamis K.
Kwa sasa Masupa nyota hawa wanaendelea na harakati mbalimbali za kimaisha kama shule na muziki pia kwa nafasi yake.
Mkali Izzo busines anayefanya vyema katika mziki wa Bongofleva aaamua kula sikukuu yake ya pasaka na watu wake wa Green city. Mkali huyo ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Tumoghele na brand ya T-shirrts za TUMOGHELE 255 ambazo zimekamata sana soko la bongo ameachia habari hiyo katika ukurasa wake wa facebook. Sow hiyo itabamba pande za Club Maisha siku ya tarehe 20 mwez wa nne jumapili ya pasaka kwa uchakavu wa 7000 tu kabla ya show na mlangoni basi mtonyo unaongezeka na kuwa kitu kizima, 10000. 
MBEYA CITY.....JUMAPILI HII YA PASAKA TAREHE  20/04/2014....NITAKUWEPO PALE NEW MAISHA CLUB....HOME SWEET HOME EASTER  SEASON....KARIBUNI TUFURAHI PAMOJA !!! #bless

SI SHOO YA KUKOSA UONE WAKUKAYA 

WANAVYOFANYA YAO

Mwanamuziki nguli wa muziki wa dansi nchini na afrika mashariki Gurumo afariki dunia. Chanzo kimoja kimetujuza kuwa mzee Gurumo amefariki mida ya saa nane mchana. 


Mzee Gulumo ashawahi kuwa mwanamuziki katika bendi kama Nuta jazz,Juwata,Ottu,Sikinde na OSS
.





Taarifa hiyo ameitoa kupitia ukarasa wake wa facebook

Nasikitika kutangaza kuahirishwa kwa shughuli ya utambulisho wa wimbo na video mpya ya Jaydee 'NASIMAMA'. Kutokana na hali tete ya bojo iliojitokeza ambayo iko nje ya uwezo wa binadamu.. LAKINI Wimbo na Video vitarushwa LEO ktk mtandao. CDs na DVD vitasambazwa kwa walengwa((Media)) hapo kesho na Jumatatu.
Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.....JayDee
A man is made up of his thoughts, what he think always makes him ! thanx kwa mnao ni support coz i always do for you...! my fans. 
PICHA YA JUU NI HAMIS K AKIFANYA YAKE KUWABURUDISHA MASHABIKI WA MJI KASORO BAHARI-MOROGORO

Siku ya jana imekuwa ni sku ambayo prodyuza mkali aliyefanya nyimbo kali za wasanii wa bongo na hasa msanii Belle 9 kutoka mji kasoro bahari amekuwa akilia na tabia za wasanii wanazozifanya katika studio zao. Triss amefanya nyimbo nyingi sana na kali ambazo ndizo zilizomleta msanii Belle 9 na kutanbulika kwa watanzania na hata nje ya nchi, kama WANITAKA, MASOGANGE, n.k 
Hiki ndicho alichokipost Triss kupitia ukurasa wake wa Facebook, jionee mwenyewe hapa







Hii ni nyimbo nyingine kutoka kwa mkongwe wa bongo fleva prof jay aliyomshirikisha diamond platnumz
download hapo kwa kubofya palipoandika download


Katika maisha watu wengi wamekuwa wakikata tamaa katika mambo mbalimbali wanayokuwa wakiyafanya kama vile masomo, biashara na hata kazi. Haupaswi kukata tamaa unatakiwa ukaze buti kwani hakuna awezae kukushusha.
Huu ni wimbo utakao kupa matumaini makubwa katika mipango mbalimbali na hata pale utakapofanikiwa ni kipi unachotakiwa kufanya.

Sikiliza na download hapo chini


Artist: Isack ft Lucy - Die hard
Song: Die hard
Producer: Jozee
Studio: Icon Record Tz