Aliyekuwa mchezaji machachari wa AC Millan, mchezaji mwenye mbwembwe za kila aina uwanjani na mitaani aelekea kukipiga AC Millan Italia.
Akiwa AC Millan atavalia jezi yenye namba 45 pamoja na Rossoneri huku akiwa amesaini mklataba wa kuitumikia timu hiyo inayong'ara katika ligi yenye umaarufu mkubwa nchini Italia na kote duniani hadi mwaka 2017.
Mwalimu wa madrasa kauliza swali kwa wanafunzi wake!
Sheikh mkuu wa TZ anaitwa nani?.Darasa zima wakanyoosha mkono na mwl akamchagua mwanafunzi mmoja huku wengine wakiendelea kunyoosha vidole,! Dogo akajibu kwa kujiamini"ostadhi juma na musoma". Mwalimu akashangaa kuona wanafunz wote wanashusha mikono., Mwalimu akaamua kuuliza, mbona mmeshusha mikono! Wanafunzi kwa pamoja wakajibu ndo ''huyohuyoooo....!

Hii ni habari njema, hii ni moja kati ya ngoma zinazowakilisha vyema, hisia za mtu aliyetemwa. Naheshimu tabia nyingi za vijana...... This is Tanzania Young DSM-Dee, with Mr Blue, goes by the name of HUJALI


Misemo mingi imekua ikisikika inayomuhusu msanii huyu anayeng'ara katika mziki wa bongo fleva, na hasa pale alipoamua kuamishia makazi yake huko Nairobi Kenya. Na hii imetokana na msanii huyu kuonekana akikubalika sana huko Kenya na kuudhirishia umma kuwa NABII hakubaliki kwao. Na hii ndio ngoma yake mpya aliyomshirikisha CP inayokwenda kwa jina la Ready to go. Big up Machozi kwa ngoma nzuri na tamu inayofaa kwa matumizi ya binadamu na hasa kwa wana Bongo fleva.

Hii ni video ya ngoma mpya ya Dj Choka a.k.a Mr Appetite baada ya ile ya kwanza ya Pamoja we can ambayo pia ilifanya vizuri katiak mwaka 2012. Waweza icheki hapa na kui pakua. Hongera the real Dj in Tanzania and East Africa kiujumla, U gonna be the NEXT DJ KHALID

Lulu (Elizabeth Michael) kuachiwa kwa dhamana


Kutokana na habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba msanii  wa filamu nchini Tanzania, Elizabeth Michael aka Lulu ambaye yuko mahabusu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam, hatotoka leo kama ilivyoandikwa na vyombo mbalimbali vya habari. Hii ni kutokana na kutotimiza masharti yote ya dhamana ikiwa ni pamoja na hati za kusafiria pamoja na dhamana ya milioni 20.

Wiki iliyopita mawakili wa muigizaji huyo waliwasilisha maombi ya dhamana kwa mahakama hiyo kuu ya Tanzania.

Wanasheria hao Peter Kibatala, Kennedy Fungamtama na Fulgence Massawe waliomba dhamana hiyo itolewe haraka kwakuwa muombaji amekaa mahabusu kwa zaidi ya miezi saba na kwamba kosa lake linaweza kupewa dhamana.

Lulu anakabiliwa na kesi ya kumuua bila kukusudia Steven Kanumba April 7, 2012, huko Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam.

Kanumba alidaiwa kuwa kwenye ugomvi na Lulu aliyekuwa mpenzi wake nyumbani kwake Sinza.


        Hii ni ngoma mpya kabisa kutoka kwa mkali wa R&B Ben Pol akiwa ameshirikiana na mwanadada kutoka Tanzania House Of Talent (THT), Linah Sanga na wimbo unaitwa ''YATAKWISHA''.
Kuwa wa kwanza kuisikiliza hapo chini na pia unaweza kudownload:



Hii ndio ngoma mpya kutoka kwa rapper Ney Wa Mitego ikiwa inaitwa ''Utavuna Ulichopanda''.
Ni ngoma nzuri sana inafaa kwa kusikilizwa na watanzania wote wanaopenda mziki wa Bongo kwani ina ujumbe mzuri ikiwa ni tofauti na ilivyozoeleka kwa msanii huyu kutoka na ngoma za kuwakandia wasanii wa Bongo kutokana na tabia zao wanazozifanya.

Sugu akiwa ndani ya EATV katika kipindi cha Friday Night Live amemshukia roma na kumuonya kuwa awe mwangalifu na anachokiandika sio kukurupuka na kuandika vitu asivyokuwa na uhakika navyo.
Katika wimbo huo kuna kipande kinasema "Pesa ndio imemaliza bifu ya Ruge na Sugu"
Sugu alienda mbali zaidi na kusema madogo wanaokuja juu kimuziki hawamuwezi na ndio maana kawatafutia wa level zao ambaye ni mwanaye Sasha.
SUGU AMSHUKIA ROMA KWA KUMTAJA KWENYE 2030:
Sugu akiwa ndani ya EATV katika kipindi cha Friday Night Live amemshukia roma na kumuonya kuwa awe mwangalifu na anachokiandika sio kukurupuka na kuandika vitu asivyokuwa na uhakika navyo.
Katika wimbo huo kuna kipande kinasema "Pesa ndio imemaliza bifu ya Ruge na Sugu"
Sugu alienda mbali zaidi na kusema madogo wanaokuja juu kimuziki hawamuwezi na ndio maana kawatafutia wa level zao ambaye ni mwanaye Sasha. Duh!



MAANA PESA NDIYO ILIFANYA TUSIWE NA TANGA NDUGU
PESA ILILETA UBAGUZI KATI YA LOYOLA NA PUGU
PESA NDIYO ILICHOCHEA BEEF YA NICE NA DUDU
NA PESA NDIYO ILIMALIZA VITA YA RUGE NA SUGU!!!

Means-

Unapozungumzia pesa basi kila mtu atakuja na tafsiri yake na mifano na matukio yake yaliyosababishwa na pesa!! ni kitu chenye maana pana sana na ni kitu kilichokaa nyuma ya vitu vingi vilivyowahi kutokea!! pengine bila pesa visingetokea!!!

familia nyingi zinaface matatizo mengi sana msiba unapotokea, hususani wa ile nguzo ya familia!!! hupelekea hata msiba unaisha na ndugu wanashindwa kukutana na kupanga lolote na hata kulala matanga hawalali, wanatawanyika !!! tumeshamzika tukafanye yetu sasa...tukilala matanga ni gharama zingine tena!!!

Kuna utofauti mkubwa sana kati ya mwanafunzi wa shule ya loyola na pugu hili lipo uchi kabisa!!!utofauti huu huleta ubaguzi ktk baaadhi ya vipaumbele...

Nilipita kwenye familia ambayo ina mtoto wa pugu na hapohapo yupo wa loyola!! baba yao na mama yao ni mmoja lakini kuna utofauti wa malezi ya kielimu na vitu vingi baina ya watoto hawa wawili!! unadhani kwanini?

Pesa ilichochea beef ya nice na dudu.....unadhani nice bila zile pesa ile beef ingekuwa kubwa kiasi kile?

Hapa sasa "pesa ilimaliza vita ya ruge na sugu"!!

-shortly ni kuwa issue ya brother sugu kuingia katika vita hii kama ilivyosemwa awali na ilivyoonekana POINT ilikuwa kuitetea sanaa, ambayo ni wasanii pia wakiwemo ndani hapo...kuwa wanachokipata hakistahili kulinganisha na kazi wanayofanya!! malipo mabovu ya show, uuzwaji mbovu wa kazi za sanaa unawafaidisha wengine kuliko wasanii,na mengine mengi sana tuliyasikia!! ambayo kimsingi yote yanaegemea kwenye kipato = pesa!!

Lakini baadae ikaja semwa na pande zote mbili zikakiri kuwa songombingo hilo limeisha baada ya pande zote mbili kukubaliana kuwa yote yaliyokuwa yakilalamikiwa yameeleweka na upande wa brother ruge umekubali kuyamaliza yote yaliyokuwa yakilalamikiwa kuwa sasa yameisha na yanatekelezwa!!

Sasa hiyo ina imply nini? kama yameisha ina maana tatizo la malipo duni ya wasanii, tatizo la wasanii kuingiza pesa nyingi na kulipwa kidogo tofauti na wanachoingiza..na yote yaliyoongelewa SASA YAMEFIKIA KIKOMO!!! BASI NI HABARI NJEMA KWA WASANII....

na hiyo yote ni nini?
- ni kuwa sasa watapata kipato sawa na haki yao!!
-wataifanya sanaa yao kwa njia sahihi na za faida kama ilivyokuwa ikihitajika ktk vita hiyo!!
-na wataiona faida ya sanaa kwa ujumla!!

KIPATO=MALIPO=PESA
BASI PESA NDO IMAMALIZA VITA YA RUGE NA SUGU!!

2030 YA R.O.M.A
NAYAJIBU NINAYOULIZWA NA YANAYOHITAJI UFAFANUZI!!!
Ni ujio mwingine wa Mwana Fa na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la FINEST, soon itakuwa hewani.
 
KAA MKAO WA KULA UJIONEE VIDEO HIYO


Diamond Platnumz – Kesho {Official HD Video}
Song: Kesho
Studio: Mj-Recordz

Chorous
Mi nataka kesho twende nikupeleke nyumbani
nataka kesho twende ukamuone mama x2


Verse 1
Kwanza kabisa ntanyonga Tai
T”shirt na Jeans ntatupa kidogo..
Unite Nasibu usiniite Dai
Asije kukuona muhuni akapandisha Mbogo…
Naukifika uagize Chai
Savanna Takila uzipe kisogo…
Kuhusu mavazi kimini haifai
Tupia pendeza ila za Hekima Logo…
 

Even though wanaponda eti we ni kicheche
Waambie ndoo chaguo langu sasa wanicheke x2


Chorous
Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2


Verse 2 
Usilete swaga za Nainai
Ukanyoa kiduku kama Moze Iyobo..
Eti shoping twende Tai
wakati Dadaangu anaduka kigogo..
Ukikuta Nguna usikatae
we zuga unapenda hata kama wa Muhogo..
Kuhusu kabila mbona Sadai
Mama angu hana noma hata kama Mgogo


Even though wanaponda eti we ni kicheche
Waambie ndoo chaguo langu sasa wanicheke x2


Chorous
Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

 
Bridge
Mama yangu mama…
Mama Naseeb mama…
Mama Diamond mama…
Mama yangu nyumbani…
Mama Chali mama…
Mama Sepetu mama…
Mama Kidoti mama…
Kwa mama Diamond nyumbani…


Chorous
Minataka kesho twende nikupeleke nyumbani
Nataka kesho twende ukamuone mama x2

Song: Wazo La Leo
Artist: Stamina Feat Fid Q 
Studio: Bongo Records 
Producer: P funk Majani 
Song Writters: Stamina (verses) & Fid Q (chorus) 

Intro... U know what majani??nice to meet you homie Its moro town baby,,, shorobwenzi 

Verse 1. (Stamina)
Elimika nyangema, maisha hayaendeshwi na nguo 
Pesa ni vazi la mgema, haliwezi kuwa na mpasuo 
Vaa uaminifu,tupa boksi la kondomu 
Hip hop haijengwi na bifu,underground usijaze fomu 
Maisha ni kujipanga, mganga usigawe irizi 
Viongozi msizuie ganja, huku mnachukua ushuru wa rizz 
Ridhiki ina kamba, ivute ili ikupe noti 
Mkulima rudi shamba,dec mbegu siku hizi hazioti 
Maisha njia panda,mtembezi chagua pa kwenda 
Uchumi vazi la bwanga,ukishuka uvishe suspenda 
Shiba kwa nia,ukiwa mlafi wa malengo 
Usikufuru we shukuru ukifaulu kila tendo 
Punguza pupa,mpendaji uingie ndoani 
Mapenzi yamevaa bukta,uswazi mapaja hadharani 
Usilale kijinga,kwenye kitanda cha ushamba 
Unaweza kuwa shabiki wa samba,na ukaishi mwembe yanga

Chorus. (Fid Q)
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono 
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono 
Neno la kuponya,lilokosa mdomo 
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo {Hilo ndo wazo la leo}
inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha. {hilo ndo wazo la leo}
usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako- {hilo ndo wazo}

Verse 2. (Stamina)
Underground panga tenzi,ustar hauji kwa promo 
Hakuna tajiri wa mapenzi,kapuku punguza ngono 
Bora uitwe mfalme jua,kwenye utawala wa kishamba 
Mapenzi yakikusumbua, tafuta daktari wa kitanga 
Vazi unaloishi, mwenyezi yeye ndio disegner 
Shetani akikushawishi, mvute kwake kama dayna 
Dunia duara,jitahidi uizunguke 
Mla bata starehe hasara,,wekeza hadhi isishuke 
Huna undugu na bakhersa,niaje aje unakula unga 
Mateja wanahitaji sensa,taifa la kesho linavunda 
Dogo jifunze,heshima sio upaparazi 
Mwambie na dada ajitunze,mlango wake asiuache wazi 
Kama unajijua ni mchoyo,basi usingoje kupewa 
Tafuta pesa kwa moyo,sio kwa ushindi wa ngekewa 
Sharo mpe salamu,the great braza kanumba 
Mwambie bongo sio tamu,na lulu bado wamemfunga 

Chorus(fid q) 
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono 
Neno la kuponya,lilokosa mdomo
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo {Hilo ndo wazo la leo}
inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha. {hilo ndo wazo la leo}
usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako- {hilo ndo wazo}

Verse 3. (Stamina)
Utamu wa ndafu ya harusi,sio wa ndoa we kilaza
Mbuzi atabaki mbuzi,hata mle hadi mkasaza 
Nchi tayari imekonda, mwananchi tafuta ulaji
Life ngumu hadi omba omba,
kidonda anafanya mtaji ukipata mazuri,
ipange kuikwepa hasara kijana vazi la msuli,
haliwezi kukuvisha busara ukiishi kwa hisia,
kila stone litakubanza cha msingi ni kuweka nia,
ujivue kuwa mtanza kata ya kijiji,
haibebi maji ya maendeleo katibu tunza mkwiji,
msuli ukishuka kimeo uchumi umeshika tama,
kwenye shavu la mlanguzi raia usilaumu chama,
shiriki kwenye uchaguzi unaweza ukavaa kinga,
ila ukafa kwa uaminifu mzinzi usigawe ujinga,
sambaza ujumbe wasifu hakuna snitch kama pesa,
ukiwa nae fanya vya maana akiondoka atakutesa, 
utamsaka usiku na mchana 

Chorus. (Fid Q) 
Hiki kijiko unachokiona, baada ya kula kwa mkono 
Ndomu usiyoiona,mpaka ukishafanya ngono 
Neno la kuponya,lilokosa mdomo 
Na hili bonge la ngoma,kwenu kwangu ni kama somo {Hilo ndo wazo la leo}
inshu usingizi wa furaha,mzinzi jenga kibanda cha angaza utoe nasaha. {hilo ndo wazo la leo}
usiishi kwa vikwazo,weka wazo kwenye vyanzo vyako- {hilo ndo wazo}