SHETTAH AELEZA SABABU ZA LADY JAY DEE KUKATAA KUFANYA NAE NYIMBO YA 'BONGE LA BWANA'

By    


Shettah Siku kadhaa zilizopita msanii aliefanya vizuri na nyimbo kadhaa ikiwemo 'Nidanganye' Shettah, alitangaza juu ya wimbo wake mpya aliopanga kumshirikisha binti machozi Lady jay dee.

Kupitia Power Jams ya EA radio, Shettah ameelezea mabadiliko yaliyojitokeza juu ya wimbo huo ambao imebidi amshirikishe Linah Sanga na sio Jide kama alivyotangaza awali. Shettah amesema hapo awali alikuwa ameshawasiliana na Lady Jay dee aliyemkubalia kufanya nae wimbo huo na Shettah alimpatia title ya wimbo ili aweze kujiandaa nayo. Mabadiliko yalikuja kujitokeza baada ya Jide kuiskia mistari ya Shettah ya wimbo huo kitu ambacho kilimsababisha kukataa kuimba katika wimbo huo kama walivyokuwa wamekubaliana mwanzo. 

"mwanzo alikuwa amekubali kabisa na nikampa title ya 'Bonge la bwana' lakini alipokuja kuiskia mistari akasema hakujua kama mimi nimeimba hicho nilichoimba so ni ngumu yeye kuimba sababu hafit kwenye idea hiyo maana hata kiumri yeye ni mkubwa kwangu, ila akasema labda niibadilishe kidogo idea kitu ambacho nimeona kitafanya na mimi nibadilike kuanzia mwanzo mpaka mwisho huku ngoma tayari iko poa. So nimeamua kuifanya na Linah na Jide kasema poa nifanye na mtu mwingine halafu yeye ntakuja kufanya nae wimbo mwingine" alisema Shettah.

Shettah anategemea kuuzindua wimbo wake huo mpya wa 'Bonge la bwana' pale Maisha club tarehe 25 mwezi huu wa November, na amewataja wasanii watakao mpa support katika show hiyo kuwa ni pamoja na Feruz, Jaffarai, Pasha, One, Stereo, Young Dee, Shilole na wengine. 

Wimbo huo umerekodiwa pale G-Records na video yake inatarajiwa kufanywa na Adam Juma wa Visual Lab Next Level.